Wastara Juma.
Habari
kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo,
zinasema kwamba Wastara amemaliza salama eda yake baada ya kufiwa na
mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari, mwaka huu.
Staa
huyo bado yupo Muscat, Oman alikoitwa na ndugu zake kwa ajili ya kukaa
eda hiyo na kupumzika baada ya kupata masaibu ya kuondokewa na mumewe
kipenzi.
KAMA MWARABU
Chanzo
kinaeleza kuwa uamuzi wa Wastara kwenda kukaa eda Uarabuni ni mzuri kwa
sababu kwa sasa yupo vizuri kiafya na mawazo ya kuondokewa na mwenzake
yamepungua.
“Ni
kweli kifo hakizoeleki lakini Wastara amejitahidi sana kutuliza kichwa
chake. Ndugu zake wamemsaidia sana, wamekuwa naye katika kipindi hiki
kwa upendo wa hali ya juu.
“Yaani
ukimuona jinsi alivyopendeza utashangaa, ni kama Mwarabu kabisa. Mungu
mkubwa sana jamani, kila mtu anafurahishwa na jambo hilo. Mungu
ataendelea kumsimamia,” kilipasha chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya
jina lake gazetini.
Wastara akiwa Uarabuni.
KUTUA BONGO