Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia
--
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.
Aidha amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwawakurugenzi wa majiji.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika katika halmashauri za majiji yaArusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.
Alisema wakurugenzi walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa yaTabora, Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.
Ghasia alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe, kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.