Monday, May 06, 2013

BIFU LA JAYDEE NA CLOUDS SASA LAFIKIA PABAYA, RUGE AAMURU CLOUDS KUTOPIGWA NYIMBO YOYOTE YA BONGOFLEVA.......


 
Akizungumza kupitia kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea yafuatayo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wiki iliyopita:
Asema vita ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahii kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.
Awaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo
Aelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo. Aaamua siku ya leo kutopigwa muziki wa Bongo Flava
Asema kuwa Clouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria
Asema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kuonana na muhusika ili kumaliza tatizo
Awaasa wasanii kukabiliana na changamoto na si kuziona kuwa ni tatizo

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 6, 2013


DSC 0001 62cc9
DSC 0002 e243a
DSC 0006 1d3df
DSC 0007 aa6d3

ANGALIA PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA

DSCN2227Hali ya eneo mlipuko ulipotokea

DSCN2220Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

DSCN2228Ulinzi umeimarishwa

DSCN2252Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

DSCN2246Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio

Sunday, May 05, 2013

RPC ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA...!!

Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu....

RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye  aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi....

 
RPC  amesema  tukio  hili  ni  la kigaidi. Amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema kuwa Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..

Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi

Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi

"WAZIRI WA ELIMU AKAMATWE NA ASHITAKIWE"... MBATIA


Baada ya Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana akamatwe na kushitakiwa. 
Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana. 
Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)  hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa Elimu.“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa, halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.
Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa sababu ni aibu kwake.

MFANYA BIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA AFARIKI DUNIA

TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika

Mfanya biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam  na tukizipata tutakuhabarisha mapema. 
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi 
Amina

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 5, 2013

.

.
.

LINA NA BARNABA WAIKACHA SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAY DEE.

Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo.
 
Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.
“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”
Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.
Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba.
source-zeddylicious

PENZI LA WEMA LAMTESA PREZZO..........!!!


Wema akiwa kwenye pozi la kimahaba na msanii wa Kenya PrezoDar es Salaam, Tanzania

BAADA ya uvumi kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kenya Prezo kuzama kwenye mahaba mazito na msanii wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu, Msanii huyo ameshikwa na kigugumizi na kushindwa kukanusha tuhuma hizo.


Prezo ambaye alifiwa na mchumba wake ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria marehemu Goldie Harvey, aliyefariki dunia February mwaka huu, juzi alishindwa kudhibitisha tuhuma hizo baada ya kuulizwa swali na kushindwa kulijibu.


Prezo ambaye yuko nchini kwa ziara ya muziki alionekana katika picha za mahaba akiwa na Wema Sepetu, hata hivyo Wema aliwahi kukanusha picha hizo na kudai kwamba walipiga wakati walipokuwa wakirekodi filamu mpya ya Wema na kwamba hana mahusiano yoyote ya mapenzi na msanii huyo.

Akiwa katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha mapenzi kilichorushwa usiku na Redio Clouds FM Prezo alishikwa na kwi kwi cha gafla baada ya kutakiwa kudhibitisha juu ya uvumi kwamba amenasa kwenye mahaba mazito na mrembo huyo mwenye skendo za kubadilisha wanaume kila kukicha.

MWANAUME AKIKOSA MTOTO HUPATA HUZUNI ZAIDI KULIKO MWANAMKE


Tofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu hao wamebaini kuwa sababu kubwa zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya zaidi wanapokosa watoto ni tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila kitu na msukumo wa familia.
Tofauti na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa ajili yao binafsi kwa asili ya kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa za utafiti huo ulioongozwa na Robin Hadley, wa Chuo Kikuu cha  Keele, ukishirikisha wanaume 27 na wanawake 81, ambao hawajapata mtoto, uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa Taasisi ya British Sociological Association,  ya Uingereza.

Saturday, May 04, 2013

SAKATA LA PADRI ALIYENASWA NA MKE WA MTU..... MAPYA YAIBUKA BAADA YA MUME KULIPONDA KANISA KATOLIKI....!!


 

LILE saga la madai ya fumanizi la Padri Urbanus Ngowi aliyekuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishiwa Makomu, Marangu limeibua mtikisiko mkubwa kwa Kanisa Katoliki nchini, .
KWANI ILIKUWAJE?
Katika habari iliyofichuliwa , Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P.

 
Mara baada ya ‘mzigo’ huo kuingia mitaani nchi nzima, mhariri wa gazeti hilo (jina linahifadhiwa) alianza kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kona mbalimbali kwa watu waliojitambulisha kuwa ni waumini wa kanisa hilo wakidai kushtushwa na tukio hilo.

VIKAO VIZITO
Habari za ndani kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi zilieleza kuwa baada ya ishu kuwa ‘hoti’, viongozi wa jimboni hapo, Jumatatu iliyopita walikaa vikao vizito kulijadili suala hilo na kulitolea uamuzi.
Ilidaiwa kuwa uongozi ulikubaliana kumwita mume wa Mama P ambaye wakati tukio hilo likitokea alikuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi.
Ilisemekana kuwa waliwasiliana na mwanaume huyo ambaye alitakiwa kuondoka Dar, Alhamisi iliyopita kwenda Moshi kukutana na viongozi hao kwa lengo la kuweka mambo sawa.
Ilidaiwa kuwa jamaa huyo ambaye amezaa na Mama P watoto wawili, alikubali kukutana na viongozi hao kwa shingo upande huku akitishia kulipeleka suala hilo mbele zaidi kwa kuwa alishalalamika muda mrefu kwamba Father Ngowi ana ukaribu wenye maswali mengi na mkewe.Tulitonywa kuwa baada ya mwenye mke huyo kulalama sana, Father Ngowi aliitwa na uongozi wa jimbo hilo kisha akaonywa lakini hakuna kilichobadilika.

PENNY...... "SINA MIMBA YA DIAMOND, NAMSHANGA ANAVYOTANGAZA KWA WATU"

HIVI karibuni, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliripotiwa akisema demu wake ambaye ni ‘prizenta’ wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki, Penny ameifungukia kauli hiyo.
Akizungumza na mapaparazi wetu kwa njia ya simu jijini Dar juzikati, mrembo huyo alionesha hali ya kupaniki huku aking’aka na kushangazwa na habari hizo za ujauzito.
 
 Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajaulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Alipoambiwa kwamba aliyesema habari kwamba yeye ana mimba ni Diamond, Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema mbali na madai ya mimba, lakini pia uhusiano wake na msanii huyo unamnyima raha kutokana na maneno ya watu.
Baada ya waandishi kujitambulisha, mahojiano yalikuwa hivi:

Funguka: Vipi, ujauzito unaendeleaje? Ni kweli una mimba ya Diamond au umeshaitoa?
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.

Ruge Mutahaba kumjibu Lady Jay Dee Jumatatu


Kwenye kipindi cha Power Breakfast kitakacho rushwa siku ya jumatatu saa mbili asubuhi Ruge Ataongelea issue ya Jay Dee ,Lady Jay Dee ameingia kwenye vita kali na Clouds Fm huku akimshambulia Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kwa madai kuwa ndio wanaokula jasho la wasanii.

MAGAZETI YA MAY 4 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

WABUNGE:: SERIKALI SASA IWANG'OE VIONGOZI NECTA


Baadhi ya wabunge na wadau wa elimu wametaka Serikali kutoishia kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, bali iwajibishe Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) kwa kufelisha wanafunzi.

 
Akizungumza kuhusu kauli ya Serikali kufuta matokeo hayo jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza alisema taarifa ya tume ingekuwa tofauti na ilivyotolewa ilikuwa isababishe vurugu nchini.

“Kauli hii ya Serikali ndiyo iliyotegemewa na wadau wa elimu, tume wangefanya vinginevyo tunge-riot (fanya vurugu), kwa sababu matokeo yaliyotolewa na Necta siyohalisi. Tume imefanya kazi nzuri na kilio cha wanafunzi kimesikika,” alisema Rweikiza na kuongeza:

“Sasa na hili nalisema bila kificho, Necta lazima wawajibishwe kwa sababu wanafunzi wanne wamejiua kwa matokeo hayo yasiyo halali, kule kwangu (Bukoba Vijijini) wanafunzi wamekata tamaa na wanaolewa. Hiyo yote ni hasara ambayo haina wa kuilipa.”

Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo Marekani, mtihani wa mwisho hauchukuliwi kama kigezo kwa sababu inategemea mwanafunzi jinsi alivyoamka siku ya mtihani na kwamba, wanatumia mitihani iliyopita kufanya tathmini yao.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...