Thursday, March 28, 2013
KIKWETE ASIMULIA ALIVYOIBA WALI JKT......!!!!
RAIS Jakaya Kikwete
amesimulia maisha yake ya jeshini, huku akikumbuka namna alivyokamatwa
na mkuu wa jiko (afande ubwabwa) akiiba wali. Rais Kikwete alitoa
ushuhuda huo wakati akifunga mafunzo maalumu ya uongozi kwa wabunge na
kuzindua mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.
Hafla hiyo ilifanyika juzi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha 832 KJ, kilichopo Ruvu, Kibaha mkoani Pwani, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.
Rais Kikwete aliwakumbusha vijana hao kwamba yeye ni miongoni mwa watu waliochukua mafunzo ya JKT kambini hapo akiwa katika Operesheni Tumaini mwaka 1972.
Rais Kikwete alisema katika mafunzo hayo alijengwa vizuri, ingawa hadi leo bado anakumbuka matukio mawili ya kufurahisha na kusikitisha akiwa kambini hapo.
Alisema tukio la kwanza ambalo hawezi kusahau ni pale alipokamatwa akiiba wali na tukio jingine ni kuhusu kifo cha askari mwenzao aliyefariki dunia baada ya kukanyagwa na trekta.
“Nawashukuru kwa kunialika katika shughuli hii, nimetembelea na kujionea miradi mbalimbali inayoendelea kufanywa hapa kambini.
“Wakati tukiwa kule nilikuwa naangalia kwa makini, hasa nilikuwa naangalia lile bweni letu, sisi tuliokuwa Kombania A mwaka ule, nimepakumbuka ingawa sasa pamekarabatiwa vizuri.
“Yapo matukio mawili ninayoyakumbuka siwezi kuyasahu hadi leo wakati nikiwa hapa kambini…(kicheko) jeshi si mchezo, nawaeleza haya mjue maisha ya jeshi hayana mzaha.
“Nakumbuka namna nilivyokamatwa na bwana ubwabwa nikiiba wali kule katika bwalo la chakula,” alisema Rais Kikwete huku wananchi na askari wanafunzi (kuruta) waliokuwapo wakiangua kicheko.
UTAJIRI WA WEMA SEPETU HUU HAPA...........!!!!
Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni
ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo
anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu.
So hebu
tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya
kuanzia mwezi June, 2012.1.
Thamani ya nyumba yake
Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha
nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds
TV.
Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi
milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za
kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012.
Sebule
Sehemu
ya nje ya nyumba
Uzinduzi wa filamu yake Superstar Katika historia ya Bongo Movies,
hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi wa nguvu kama wa filamu ya
Wema ambayo hata hivyo haijawahi kutoka, Supastar. Katika uzinduzi
huyo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria,
Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Giraffe
Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo
na Omotola. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushindwa kufika kwa wakati.
Awali
ulifanyika uzinduzi wa filamu hiyo yenye mastaa kibao akiwemo yeye
mwenyewe, TID, Shetta, Mwinyi Machozi, Chaz Baba, Barnaba na wengine
kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako mastaa wote wa orodha A
nchini walihudhuria huku Shaa na Shilole wakiwa miongoni mwa wasanii
waliotumbuiza.
Rais Kikwete azindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi na Malaria Mwaka 2012.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti
wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe
Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki.
Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama
Fatma Mrisho na
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William
Lukuvi.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akinyanyua juu baada ya taarifa ya utafiti wa viashiria vya
ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo
Pinda. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi
(TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
MBUNGE SALIM HEMED HAMIS AANGUKA GHAFLA
Mbunge wa chambani (CUF) Visiwani zanzibar Salim
Hemed Hamisi ameanguka ghafla akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya
nje na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar
es salaam wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake
Mbunge
huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya
afya yake amefikwa na dhahama hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa
kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha
mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na
matibabu zaidi.
Mwenyekiti
wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward
Lowasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wednesday, March 27, 2013
SIKU CHACHE BAADA YA KUFUNGA NDOA JACK WA CHUZ YADAIWA KAIBA MUME WA MTU
Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa blog hii
kribuni tulikuletea habari juu ya Jack wa Chuz kufunga ndoa na kubadili
dini kwa habri zilizoko ni kwamba baada ya saa 48 tu Jack kufunga ndoa
ymekuja mapya kabisa baada ya dada Mariam Omary anayedai Jack Chuz
kamchukulia baba(Gardner Dibibi) watoto wake akiwa na mwanaye.
Mwanamke huyu mwenye jina la Marium
Omary inadaiwa kuwa na mahusiano na Gadner Dibibi kwa muda wa miaka
mitatu sasa na kufanikiwa kupata mt0to mmoja wa kiume.
Dada huyu ambae anishi Kigogo jijini
dar es salaam alisema siku ya tukio ya ndoa ya Gadner alimuaga kuwa
anasafiri anaenda Morogoro hivyo hatakuwepo dar lakin baada ya muda dada
huyu alipata taarifa kutoka kwa watu kuwa mumewe anafunga ndo na
mwanadada Jack wa Chuz
Dada huyu alialamika na kusema kuwa
Jack wa Chuz anajua kila kitu kuhusu yeye na Dibibi na kusema
“Hakuna asichokijua kati yangu na
Dibibi, kwa usalama wake Jack aniachie mume wangu,” alilalama mwanamke
huyo.
Baada
ya Jack kulizwa swala hili alisema hivi ‘’baba wa mtoto anayemjua ni
mama peke yake na isitoshe kuzaa naye isiwe sababu kwani yeye hakumuoa’’
Na Dibibi naye alikuwa na haya ya
kusema
“Alikuwa demu wangu na kuzaa mtoto
isiwe sababu. Hata hivyo, ukweli wa baba wa mtoto anayejua ni mama.
Sikumtolea mahari wala kumvalisha pete ‘so’ hana kizuizi na ndoa yangu,”
alisema jamaa huyo kisha akakata simu’’
KWA WALE WAPENDA TATOO ANGALIA MADHARA YAKE KWENYE MIILI YETU
Hii ni kwa wale wote wapenda kujichora miili
ya kwa inayojulikana kama tattoo
UJUMBE WA FIFA KUSIKILIZA WAGOMBEA TFF APRILI 16
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika
kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe huo ambao moja ya shughuli zake
kuwasikiliza wote walioenguliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF
na hawakuridhika na uamuzi huo, utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka
huu.
Kwa mujibu wa barua ya
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar
Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na kutoa ripoti kwa
mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa mwongozo.
Ujumbe huo utakutana na pande mbalimbali
zinazohusika wakiwemo wagombea, kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia
ujumbe huo unatarajia kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi wa viongozi wa TFF ulikuwa
ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya
baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika kuwa hawakutendewa haki na
wangependa shirikisho hilo liingilie kati.
‘Siri ya Kuuawa Zitto Yafichuka’ – Sio Kweli.
Katika
gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna
habari yenye kichwa chenye maneno
‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na
vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa
atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa
kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na
wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja,
sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane
na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu
kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio
tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi
kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela
Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba
mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
TIGO yazindua Ofa ya bei moja kupiga simu kwenda mitandao yote
Meneja
wa Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani
ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi, kushoto kwake
Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma .
Mtaalam
wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda
mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya
nchi.
Albam ya Justin Timberlake yauza kopi 968,000 katika wiki ya kwanza
Albam mpya ya
Justin Timberlake, “The 20/20 Experience” imekamata nafasi ya kwanza
kwenye Billboard 200 chart, kwa kuuza kopi 968,000 katika wiki yake ya
kwanza, kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.
“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.
Mauzo huzo hayo ya “20/20′s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.
Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.
“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.
Mauzo huzo hayo ya “20/20′s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.
Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.
Subscribe to:
Posts (Atom)