Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa
Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati) kweye moja kati ya
studio za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Picha
juu na chini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakiongozwa na
Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa
Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma
walikohudhuria sherehe za kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki
Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo
kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa
Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa
Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati
alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Chakula , FAO, Bw. Jose Graziano da Silva kutia saini katika kitabu cha
wageni mshuhuri wakati alipotembelea Ofisi za FAO mjini Rome Machi 20,
2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya
mazungumzo yao wakati alipotembelea makao makuu ya FAO mjini Roma,
Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).