Sunday, March 03, 2013

Tume ya Wajumbe 15 iliyoundwa na Waziri Mkuu ya kuchunguza Matokeo CSEE 2012 hii hapa.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana Jumamosi, Machi 2, 2013 amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Waziri Mkuu amezungumza na wajumbe wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk  Shukuru Kawambwa. 
Amesema kwa  mujibu wa hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa kuangalia ni sababu zipi zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya, mserereko wa kushuka umekuwa ukiongezeka kwa sababu gani, usimamizi katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu na uhamishiwaji wa sekta ya elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
Vilevile, watatakiwa kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano uliopo kwenye mitihani inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mitihani hiyo; kuangalia mazingira ya kufundishia, mfumo wa upimaji, usimamizi na uendeshaji, na kutokuwepo kwa chakula shuleni kunachangiaje kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi katika masomo yao.
Tume hiyo yenye wajumbe 15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi iwe imekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu. 
Tume itaongozwa na Prof. Sifuni Mchome wa Tume ya Vyuo Vikuu, na Makamu wake atakuwa Bi. Bernadetha Mushashu (Mbunge wa Viti Maalum – Kagera).
Wajumbe ni Bw. James Mbatia (Mbunge wa kuteuliwa), Bw. Abdul J. Marombwa (Mbunge wa Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu – UDSM), Bibi Honoratha Chitanda (CWT), Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw. Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
Wangine ni Bw. Rakhesh Rajani (TWAWEZA), Bw. Peter Maduki (CSSC), Mwl. Nurdin Mohamed (BAKWATA), Bw. Suleiman Hemed Khamis (Baraza la Wawakilishi, Zanzibar), Bw. Abdalla Hemed Mohamed (Chuo Kikuu – SUZA), Bw. Mabrouk Jabu Makame (Baraza la Elimu Zanzibar na Bw. Kizito Lawa (Taasisi ya Kukuza Mitaala).

Mkutano wa CUF Jimbo la Kwamtipura mjini Zanzibar


Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu wakushoto akiwa na Mkurugenzi wa Habari,Uwenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF Salum Abdallah Bimani wakisikiliza kwa makini risala ya vijana wa jimbo la Kwamtipura katika mkutano wa hazara uliofanyika katika kiwanja cha mpira kwamtipura.
Wananchi wa Jimbo la Kwamtipura wakisikiliza kwa makini hutuba ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu hayupo pichani katika Mkutano wa hazara uliofanyika huko ktk kiwanja cha mpira kwamtipira
Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu akihutubia wananchi wa Jimbo la Kwamtipura katika Mkutano wa hazara uliofanyika ktk kiwanja cha mpira kwamtipira.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). 

Makamu wa Rais Dkt. Bilal Kufungua Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi Mkoani Mara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa  Miradi ya  Maendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe  04/03/2013 mkoani Mara.
Pamoja na shughuli nyingine, siku ya  Jumatatu tarehe 04 Machi 2013 akiwa mkoani humo, Mhe. Makamu wa Rais  ataweka  jiwe la msingi kwa ajili ya  ukarabati wa barabara ya kutoka mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mara hadi  Musoma yenye urefu wa kilomita 85.5.  Barabara ambayo ujenzi wake utawekewa jiwe la msingi ni sehemu ya Barabara ya Mwanza – Nyanguge – Makutano – Musoma ambayo ni kiungo muhimu  na nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.  Hivyo kukamilika kwake ni fursa nyingine nzuri ya kuibua uchumi wa nchi yetu na ukanda huu.
Jumanne ya tarehe 5 Machi 2013 asubuhi Mhe. Makamu wa Rais atazindua Kivuko cha Musoma kinachotoa huduma kati ya Musoma na Kinesi.  Siku hiyo hiyo mchana Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) zilizoko eneo la Old Customs katika barabara ya Lake Side, Musoma.
Uzinduzi wa miradi hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri na makazi kwa wananchi wake. Aidha, uzinduzi  wa Kivuko cha Musoma (MV Musoma) kinachotoa huduma kati ya Manispaa ya Musoma na Kinesi Wilayani Rorya ni utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais baada ya kupokea ombi la Kivuko kutoka kwa wakazi wa Musoma na vitongoji vyake.

Saturday, March 02, 2013

Siku chache baada ya Wema sepetu kutangaza nafasi za kazi mrebo huyo ashangazwa na wingi wa Emails

Wema Sepetu ashangazwa na wingi wa email anazopata baada ya kuanzisha kampuni na kutangaza ajira
Hivi karibuni Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu alizindua rasmi ofisi za kampuni yake iitwayo Endless Fame Films zilizopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Uzuri wa ofisi zake unadaiwa kuifanya kampuni yake kuwa ya kwanza nchini ya aina hiyo yenye ofisi za nguvu zaidi. Baada ya kutangaza nafasi za kazi mbalimbali wiki hii, Wema ameshangazwa na wingi wa email alizopokea kiasi cha kupost picha kwenye Instagram yenye maneno: da emails omg... im tryng ma best to reply ol of dem....

MASTAA WA KIKE WAITWA IKULU

 
KUSOMA HABARI HIIBOFYA HAPA

HEBU CHEKI MADEMU WAMEMPAKATA Q CHILLA ..!

ZAIDI YA ABIRIA 50 WA BASI LA SUMRY LITOKALO SUMBAWANGA KUJA MBEYA WANUSURIKA KUFA KWENYE AJALI ILIOTOKEA MPAKANI MWA SONGWE NA MBOZI MBEYA




















MAJERUHI MUSA KAPINUKE



MAJERUHI CHALES KAUZENI  15

MUUGUZI ELMAT KAKAKU AMESEMA WAMEPOKEA MAJERUHI 47 KATI YA HAO WAWILI WAMEPELEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA HALI ZAO KUWA MBAYA ZAIDI




HABARI KAMILI YA AJALI HII TUTAWAFAHAMISHA BADO TUNAFUATILIA

PICHA NA MBEYA YETU

Mshindi wa Tigo Smartcard Promotion Julius Kanza awasili nchini Hispania.

 
Mshindi wa Tigo Smartcard Promotion Bw. Julius Raphael Kanza akiwa Madrid Hispania tayari kusubiri pambano la el classico kati ya Real Madrid na Fc Barcelona litakalofanyika kesho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Julius Kanza akitembelea sehemu mbalimbali za jiji hilo.

DStv REWARDS YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA: AHMED SALIM SALEH ASHINDA Tshs.5,000,000



Ahmed Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
Katika muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh, mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.   Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)
Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.
DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.   Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka “mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.
Mshindi wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.

WANAO DAI KUWA LULU MICHAEL KAFANYIWA SHEREHE YA KUTOKA GEREZANI NI WAONGO NA WANAMPANGO WA KUMKWAMISHA KISHERIA..:...FAMILIA YA LULU YANENA



Kulipuka kwa habari kuwa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefanyiwa sherehe na kigogo baada ya kutoka Segerea, Dar kwa dhamana, familia yake imecharuka na kudai kuwa hakukuwa na jambo kama hilo wala haifikirii kufanya hivyo

Habari za uhakika zilidai kuwa Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mara baada ya kuachiwa kwa dhamana Januari 26, mwaka huu, kuliibuka minong’ono kutoka kwa marafiki zake mbalimbali walioelezwa kuwa walitaka kumfanyia pati lakini ndugu walikataa.

Ilielezwa kuwa licha ya ndugu hao kukataa kumfanyia sherehe ndugu yao (Lulu), bado kuna kikundi cha watu kiliendelea kueneza taarifa za kizushi kwamba lazima kuwe na sherehe ya kumpongeza baada ya kutoka gerezani.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya familia ya Lulu zilieleza kuwa taarifa zilizosambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba alifanyiwa bonge la pati na kikundi hicho kama madai ya awali yalivyokuwa, hazikuwa na ukweli wowote na mbaya zaidi zililenga kumjengea Lulu mazingira magumu ya kisheria.


Akizungumza na mwandishi wetu kwa sharti la kutochorwa jina , dada wa Lulu alisema kuwa familia ilikerwa kupita maelezo na kuwepo kwa taarifa hizo huku akisisitiza kwamba hazina ukweli wowote.

“Sisi kama familia hatujamfanyia wala hatufikirii kumfanyia sherehe ya aina yoyote kwa ajili ya kumpongeza. Tunaomba ieleweke hivyo na hao wanaoeneza habari za uongo waache haraka, hatuzipendi,” alisema dada huyo.

HATIMAYE SERIKALI YAANZA KUJENGA KIWANDA CHA GESI MTWARA


Rais Jakaya Kikwete akiangalia shughuli za uzalishaji umeme hivi karibuni, baada ya vutanikuvute ya muda mrewfu Serikali imeamua kujenga kiwanda cha gesi mkoani Mtwara
                                                      ***********
 
HATIMAYE ujenzi wa kiwanda cha kusafisha gesi kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam umeanza mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation (CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema Maswi.

KILIMANJARO MARATHON YAZINDULIWA

Maandalizi ya Mbio za Nyika za Kilimanjaro Maarufu kama Kilimanjaro Marathon 2013 yanafikia kiele hii leo na kesho ndio kivuvumbi na jasho wakati maelfu ya wanariadha na watu wa kawaida wakitimua vumbi katika mbio hizo zinazofanyika katiua mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Pichani ni baadhi ya wakimbiaji wakijiandikisha kwaajili ya kushiriki mbio hizo zitakazo fanyika Machi 3,2013 mjini Moshi na zitakuwa za makundi mbalimbali 42KM, 21KM na 5km Fun Run.
Makundi mbalimbali katika Jamiui nayo yanashiriki ikiwa ni pamoja na walemavu ambao pichani wakiwa katika banda la kujiandikishia.
Maofisa watakao simamia Mbio hizo Machi 3, 2013 wakiwa Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi kuchukua vifaa.
Mbio za kujifurahisha kwa watoto na watu wazima zipo na hapa wakijiandikisha.
Baadhi ya wadhamini wakiwa tayari wamesha pamba mabanda yao ndani ya Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi.
Mitaani napo Mabango ya Mbio hizo yamewekwa

Rais Obama awa miongoni mwa viongozi walioalikwa katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Kenya.


Rais Barrack Obama wa Marekani amekuwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa dunia walioalikwa katika hafla ya kuapishwa kwa rais wa nne wa Kenya.
Mkuu wa Huduma za Jamii Francis Kimemia serikali imewaalika viongozi kama vile Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon na Mkuu wa Mataifa ya umoja wa Ulaya.
Pia wamealikwa marais wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni pamoja na rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Rais mpya wa Kenya  anatarajiwa kuapishwa kuchukua madaraka hapo Machi 3 mwaka huu, ikiwa ni wiki tatu baada ya wakenya kufanya uchaguzi.
 

Wafanyakazi Ikulu Waadhimisha Siku ya Mazingira Afrika kwa Kufanya Usafi wa Mazingira.


Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (mwenye blauzi ya kijani) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Julius Mogore(mbele)   wakiongoza shughuli za usafi kuzunguka maeneo ya Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 1, 2013 katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika. Siku hiyo itaadhimishwa kitaifa siku ya Jumapili.


Picha zingine zinaonesha  Wafanyakazi wa kila kada Ikulu bila kujali nyadhifa zao  wanafanya kazi bega kwa bega kuhitimisha Siku ya Mazingira Afrika kwa kufanya usafi.(PICHA NA IKULU).

Rais Kikwete aongoza kikao cha baraza la Mawaziri leo jijini Dar.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao  cha baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1, 2013.(PICHA NA IKULU).
 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...