Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Thursday, April 23, 2015
SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 23, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
VOLCANO YALIPUKA CHILE
Volcano aina ya Calbuco imelipuka kwa muda mfupi huko ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 40. Watu waliokuwa wakiishi maeneo jirani na ulikotokea mlipuko wa Volcano hiyo wamelazimika kuyahama makazi yao.
Picha
za televisheni zilionyesha wingu zito na majivu vikipanda hewani umbali
kilomita kadhaa angani katika jimbo la Los Lagos kusini mwa Chile.
Mamlaka
nchini humo zimetoa tangazo la hali ya hatari kwa wakazi wote ambao
wapo umbali wa kilomita la mlipuko wa Volcano hiyo huku safari za ndege
kuelekea eneo hilo zikiwa zimeahirishwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
HALI MBAYA YEMEN...!!!
Shirika
la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya
nchini Yemen, huku Mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha
siku tisa zilizopita.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini
humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa
alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni
upelekaji wa huduma za kitabibu.
Awali Saudi Arabia ilisema
itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi
nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza
mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour
Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande
mbili. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
TIMU 4 ZATINGA NUSU FAINALI ULAYA
Timu
nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani
Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na
Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.
Wakicheza katika uwanja wao wa
nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika
ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez
almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico
Madrid.
Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo
Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake
lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila
kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa
wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Monday, April 20, 2015
CHADEMA: ZITTO NI ADUI YETU NAMBA MOJA...!!!
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake
namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and
Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema
haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.
“Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili
na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono
Ukawa halafu mnawakaribisha?
“Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto.
Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana
kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni
aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki
Ukawa,” alisema Mnyika.
Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ANGALIA PICHA ZA MAMIA YA WATU WALIOHUDHURIA MKUTANO WA ACT-WAZALENDO MKOANI MWANZA
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe,
akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha jijini humo.
Umati wa watu ukiwa katika mkutano wa ACT-Wazalendo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
(Picha na Said Powa)
SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 20, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
LOWASSA ATHIBITISHA UBORA WA AFYA YAKE
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa akiwa katika matembezi ya kupinga mauaji ya albino.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, jana alithibitisha kwa vitendo kuwa afya yake iko safi baada ya kutembea umbali wa kilomita tano kwa miguu kwenye matembezi ya kupinga mauaji ya albino nchini.
Kwa muda mrefu, Lowassa ambaye ni mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, amekuwa akidaiwa kuwa na matatizo ya afya na kuwa hawezi kuhimili mikimiki ya kampeni na shughuli nyingine zinazohitaji nguvu.
Lakini matembezi ya jana yaliyoongozwa na Lowassa kuanzia Uwanja wa Taifa wilayani Temeke mpaka viwanja vya TCC Chan’gombe na kutumia dakika 25, yamedhihirisha vinginevyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UCHINA KUWEKEZA MABILIONI PAKISTAN
Rais wa China Xi Jinping ameanza ziara ya siku mbili nchini Pakistan hii leo.
Bwana
Xi atazindua mpango wa uwekezaji wa kichina wa gharama ya dola bilioni
50 ambao Pakistan ina matumaini kuwa utasuluhisha tatizo lake ya
nishati.
Mpango huo unaofahamika kama barabara ya uchumi ya China
na Pakistan ni pamoja na barabara , reli na mabomba ya jumla ya umbali
wa kilomita 3000 kutoka mji wa bandari wa Gwadar nchini Pakistan hadi
mji wa ulio mashariki mwa China wa Kashgar.
Waandishi wa habari
wanasema kuwa lengo la China ni kuongeza ushawishi wake wa kiuchumi kwa
Pakistan ili kulegeza ule wa Marekani na India. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SULUHU YATAKIWA KUHUSU WAHAMIAJI
Waziri
mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura
cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji wanaoangamia
kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia ajali
ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti
kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha
Lampedusa, nchini Italia.
Manusura 28 wa janga la hivi punde
kwenye bahari ya Meditaranean walitarajiwa kufikishwa kisiwani Sicily
alfajiri ya Jumatatu. Hadi kufikia usiku, ni miili 24 iliyokuwa
imeopolewa, na maafisa wa usalama kwenye pwani ya Italia, wakaipeleka
kisiwani Malta.
Ni vigumu kuhakikisha idadi ya watu walioanza
safari kwenye boti hiyo kutoka pwani ya Libya. Lakini walionusurika
wanasema walikuwa kati ya watu 500 na 700 kabla ya kupinduka kilomita
mia mbili kutoka Lampedusa, kwenye maji ya Libya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)