Spika
wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa
wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.
Kulingana
na gazeti la daily Monitor,Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa
sherehe ya kitamaduni ambayo inapinga ukeketaji ilioandaliwa na mfuko wa
umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo TzWednesday, December 03, 2014
MLIPUKO MKUBWA MOGADISHU
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
DROO YA KOMBE LA AFRIKA KUFANYIKA LEO
Mabingwa
wa zamani Zambia na waandalizi wa kombe la bara Afrika Equitorial
Guinea ni miongoni mwa timu zitakazoorodheshwa katika droo ya kombe hilo
la mwaka 2015 Jumatano usiku.
Shirikisho la soka barani Afrika
CAF tayari limezigawanya timu hizo 16 katika makundi vyungu vinne vya
kinyang'anyiro hicho cha january 17 hadi februari 8.Hatua hio ilifanyika kulingana na utendaji wa timu hizo katika awamu tatu ya michuano hiyo na mechi za kufuzu katika kipindi hicho hicho.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilitiliwa mkazo ni matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.
Droo hiyo ambayo itabuni makundi manne yanayoshirikisha timu moja moja kutoka kila chungu itafanyika mjini malabo jumatano usiku. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Ghana na Ivory Coast ni timu nyengine kubwa huku washindi wa pili wa mwaka 3013 Burkina Faso wameorodheshwa katika kundi la Pili.
2015 Nations Cup :Timu zilivyowekwa.
Pot 1: Equatorial Guinea, Ghana, Ivory Coast, Zambia
Pot 2: Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria
Pot 3: Cape Verde, South Africa, Cameroon, Gabon
Pot 4: Guinea, Senegal, DR Congo, Congo
Monday, December 01, 2014
RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA ASSAD KUWA CAG MPYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi,
2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi
wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
BOKO HARAM WAVAMIA MIJI MIWILI NIGERIA
Watu
wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi
katika miji miwili eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
La kwanza lilikuwa la kujitoa mhanga pamoja na shambulizi lengine katika kituo cha polisi cha Damaturu.Wenyeji wa mji wa Maiduguri walielezea kusikia milipuko miwili kwenye soko moja.
Mashambulizi mengine ya kujitoa mhanga eneo hilo wiki iliyopita yaliwaua zaidi ya watu 70.
Mapema leo Jumatatu watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliteketeza kituo cha polisi katika mji wa Damataru kilicho umbali wa kilomita 100 Magharibi mwa mji wa Maiduguri.
Inaarifiwa watu 5 wameuawa katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotokea katika soko lililokuwa na watu wengi.
Mjini Damaturu , milipuko na milio ya risasi ilisikika huku wanamgambo hao walipokuwa wanashambulia mjini huo.
Boko Haram imeahidi kubuni dola ya kiisilamu katika maeneo ambayo kundi hilo linadhibiti.
Milipuko hio ilitokea Jumatatu katika soko la Maiduguri , mji mkuu wa jimbo la Borno ambayo ilisababishwa na wasichana wawili waliojilipua.
Takriban watu 32 walijeruhiwa katika milipuko hio. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
ICC YAKATAA OMBI LA MUASI LUBANGA
Mahakama
ya kimataifa ya ICC mjini Hague, imetupilia mbali ombi la rufaa
lililowasilishwa na muasi wa zamani nchini DRC Thomas Lubanga dhidi ya
hukumu aliyopewa kwa makosa ya kuwatumia watoto kama wanajeshi.
Viongozi
wa mashtaka walisema wavulana wadogo wenye umri wa miaka 10 walitekwa
nyara na kusajiliwa kama wanajeshi DRC katika vita hivyo vilivyoanza
mwaka 1999.Wasichana nao walitumiwa kama watumwa wa ngono.
Mnamo mwaka 2012, Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hio.
Aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la (UPC), ambalo lilikuwa la kabila la Hema ambalo lilihusika katika vita eneo la Ituri Mashariki mwa DRC.
Mahakama ilimpata na hatia kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na kuwatuma kwenda kumpigania. Alihukumiwa kifungo cha miaka 14.
Kundi la UPC, lilikuwa moja ya makundi sita ya wapiganaji waliopigana kudhibiti eneo lenye utajiri wa madini la Ituri hadi mwaka 2003.
Mgogoro ulianza kama mvutano wa kupigania mali asili, ingawa baadaye ilipanda daraja na kuwa vita vilivyohusisha jeshi la Uganda.
Kadhalika mgogoro huo uligeuka na kuwa vita kati ya jamii za Hema na Lendu ambapo takriban watu 50,000 waliachwa bila makao. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Sunday, November 30, 2014
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 30, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
HONGERA DIAMOND: ATWAA TUZO 3 ZA CHANNEL O AFRIKA KUSINI
Diamond akiwa na tuzo.
MSANII
Naseeb Abdul 'Diamond Platumz' ametwaa tuzo tatu za Channel O usiku wa
kuamlia leo nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni; Most Gifted new comer,
Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number
One! Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
TAZAMA PICHA ZA AJALI YA HELIKOPTA ILIYOANGUKA JANA JIJINI DAR
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar, Ilala jijini Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
ZIARA YA KINANA MTWARA MJINI
Vijana
wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali
mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
Wananchi wa Mikindani mkoani Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)