Katika
mazingira ya kutatanisha, jana Jumapili Novemba 02, mwaka huu vurugu zimekatisha mdahalo
uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku
baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa
ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za hapa nchini ulivurugika
kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake.Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka salama nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo jijini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz