JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu
makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu
iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na.
TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014
akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki
iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.

Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.
Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata
mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika
kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za siri. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz