ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi,
hata raia wake. Kunahitajika jitihada
za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea
Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu
sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya
kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu
hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi
makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na
matukio kama haya.
Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika
kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni '
Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.