Matokeo
ya kidato cha nne yanayotarajiwa kutangazwa leo, yamezidi kuzua mapya
baada ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni
iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo
likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli.
Kanuni
iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia
kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini
Dodoma.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake
wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
“Wakati
yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54,
kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa
madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
Chanzo
chetu kilieleza kuwa, katika kikao hicho, kulikuwa na mvutano kuhusu
kanuni ipi itumike ili kuwaokoa wanafunzi hao alama zao zisishuke.
Baada
ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda tena kuyafanyia kazi
matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa asilimia zaidi ya 20 hadi
kufikia asilimia tisa.
“Kwa
sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo
kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu kweli,” kilisema chanzo hicho na
kuongeza:
“Ukijaribu
kuangalia, Necta wanasimamia kanuni, lakini wakati mwingine inabidi
mtu uangalie hali ilivyo, kwa sasa watu wanaangalia zaidi mwitikio wa
wananchi utakavyokuwa haya matokeo yakitangazwa badala ya kuangalia
vitu vya msingi,” kilisema chanzo hicho.