Monday, July 28, 2014

MBEYA CITY, NDANDA FC, STAND UNITED: 'ONYESHENI BINSLUM HAKUKOSEA KUWADHAMINI'


Ibrahim Bakari 

Ninataka kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Bin Slum, Nassor Bin Slum nikiwa na sababu moja kubwa, BinSlum hakutaka biashara za timu kubwa, alichoangalia ni kuzisaidia timu ndogo zilizopanda Ligi Kuu.

Katika siku za karibuni, klabu za Mbeya City ya Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga, zimepata udhamini wa mamilioni na Nassor BinSlum kupitia kampuni yake ya BinSlum.
BinSlum alianza kwa kuidhamini Coastal Union ya Tanga ambayo alisema ameondoka kwenye timu hiyo kutokana na majungu.
Sitaki kuzama kwa hayo yaliyotokea Coastal Union, lakini naipongeza kampuni hiyo inayojishughulisha na uuzaji wa betri na matairi ya magari.
Ninataka kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Bin Slum, Nassor Bin Slum nikiwa na sababu moja kubwa, BinSlum hakutaka biashara za timu kubwa, alichoangalia ni kuzisaidia timu ndogo zilizopanda Ligi Kuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Wadhamini wamekuwa na tabia ya kuangalia timu kubwa kubwa kama Simba au Yanga. Hizi tayari ziko juu, zina rasilimali za kutosha kujiendesha wakiwamo wanachama, lakini huku kwingine hakuna.
Mbeya City ambayo ilionyesha makali yake hata kushika nafasi ya nne katika Ligi Kuu, inastahili kupata udhamini wa kweli kwa kuwa wachezaji wake wameonyesha wana nia.
Hata ushiriki wao wa michuano ya Nile nchini Sudan, ilionyesha kuwa inaweza, kinachotakiwa ni kupata ‘sapoti’.
Baada ya kupata udhamini wa BinSlum, ninaamini, Mbeya City, Ndanda FC na Stand United zitaonyesha kandanda ya ushindani katika mechi za Ligi Kuu. Inakera kuona timu zinafungwa ovyo ovyo na kuondoa msisimko wa ligi.
BinSlum ameingia mkataba wa miaka miwili na Mbeya City wenye gharama ya Sh360 milioni na kila mwaka timu hiyo itakuwa inapewa Sh180 milioni.
Stand United na Ndanda FC kila mmoja amedhaminiwa kwa Sh50mil. Kutokana na hilo, Stand United watavaa jezi zenye logo ya Double Star Tire sanjari na Ndanda FC.
Sasa, hapa nina mawili, kwanza nilikuwa navuta muda kuona mdhamini mwingine anajitokeza nitoe pongezi zangu za jumla, lakini kwa hili hapa, naamini soka itakuwa ya ushindani, kwamba timu zilizopanda Ligi Kuu hazitatetereka sana. Pia kuna udhamini wa Azam pamoja na Kampuni ya Vodacom.
Kingine ni kwamba, timu zilizopata udhamini zisiwaangushe walioamua kuingiza fedha zao kwao.
Hakuna mtu ambaye anaweka fedha mahali ambako hakuna hata lepe la ushindani, na ni rahisi sana kwa mdhamini kughairi kuendelea kuidhamini timu goigoi.
Ndiyo maana kuna wakati niliwahi kuandika hapa kuwa timu zilizopanda Ligi Kuu ziige ilichokuwa ikifanya Mbeya City, kwani imepanda Ligi Kuu na haikufanya mzaha hata zilipokuja timu kubwa, Simba, Yanga, Azam haikutetereka.
Siri kubwa ni kutokuwa wanyonge na kuonyesha soka ya ushindani hata zinapokuja timu kubwa.
Hiyo itasababisha kuibuka kwa wadhamini wengine. Mbeya City wameonyesha njia na hata wadhamini akiwamo BinSlum kujitokeza sasa na hawa wengine iwe hivyo.
Hatutarajii kuona timu zinapata udhamini halafu zinavurunda, haiwezekani wachezaji wakapata chao halafu wasicheze kwa moyo, itavunja nguvu wadhamini, hilo nalisisitiza.
Ninaamini wadhamini wengine watatokea na timu kupata fedha zitakazowapa chachu ya kuleta ushindani katika mechi zao na isifike hatua wadhamini kusikitikia udhamini wao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...