Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja
na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa
marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya
Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii
wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni yake ya Proin Promotions
ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii
wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana
na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu
yake ya “Foolish Age”.
Jengo
jipya la kisasa la Kampuni ya Proin Promotions ambalo linatarajiwa kuzinduliwa
rasmi hivi karibuni likionekana kwa nje. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
========= ======= =====
FILAMU YA “FOOLISH AGE” YAIKUTANISHA LULU NA BODI YA
FILAMU.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
KAMPUNI
ya Proin Promotions imewasilisha filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age”
Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa
marekebisho filamu hiyo inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi
karibuni.
Bodi
ilifikia hatua ya kuwaita wahusika yaani Proin Promotions na Elizabeth Michael (Lulu)
kwa ajili ya kufanya majadiliano kuhusu maudhui na maadili katika filamu hiyo
kabla ya kufanyia maamuzi.
Katika
majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya baadhi ya
marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa umma, pia Bodi ya
Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia kifungu cha 14 cha Sheria ya
Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu,
matangazo na maelezo yote na kile cha 24
(1) (d, n na t) cha Kanuni za
sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua mambo yanayotakiwa na yale
yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo imekwenda kinyume.
Kwa
upande wake Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Bi. Gift Msuya
alikubaliana na ushauri uliotolewa na Bodi ya Filamu na aliiomba Bodi itoe muda
kwao kwa ajili ya kufanyia marekebisho katika filamu hiyo. Naye
msanii Elizabeth Michael (Lulu) aliieleza Bodi ya Filamu kuwa Filamu hiyo
aliitengeneza muda mrefu na kwa sasa atazingatia maelekezo ya sheria, Kanuni na
taratibu hususani katika eneo la maadili. Aidha alikiri kuwa ni kweli maeneo
yaliyobainishwa kweli yanahitaji marekebisho.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Fissoo alimalizia kwa kuishauri Kampuni hiyo
kutotumia filamu hiyo katika uzinduzi wa kampuni yao hadi hapo watakapofanyia
marekebisho katika baadhi ya maeneo muhimu ndani ya filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment