Sunday, November 30, 2014

RAIS KIKWETE ' NIMEPONA SARATANI'

Rais kikwete akitoa hotuba yake kwa taifa .Amesema kuwa amepona saratai ya kibofu.
  Rais Jakaya Kikwete amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani. Rais Kikwetemwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WALIOKUFA KWA EBOLA WATIMIA 7,000



Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola, karibu wote Afrika Magharibi.
Hao ni watu zaidi ya elfu moja kuliko idadi iliyotangazwa na WHO Jumatano tu.
Vifo vingi zaidi vimesajiliwa Liberia.
WHO inasema watu zaidi ya 16,000 wameugua Ebola hadi sasa.
Waandishi wa habari wanasema kuongezeka kwa idadi ya waliokufa siyo lazima inamaanisha ugonjwa unazidi kutapakaa kwa kasi kwa sababu takwimu nyengine ni za zamani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, November 29, 2014

SWAPO YAELEKEA KUSHINDA TENA NAMIBIA

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa Namibia yanaonesha kuwa chama tawala cha SWAPO kimeshinda kwa kura nyingi.
SWAPO imetawala Namibia tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka wa 1990.
Lakini wanasaiasa wa upinzani kwa mara nyengine tena wanataka kura ibatilishwe, wakidai kuwa kanuni zilikiukwa na wapigaji kura waliendelea kupiga kura hata baada ya muda uliowekwa.
Mahakama makuu katika mji mkuu, Windhoek, yalitupilia mbali madai ya kuahirisha uchaguzi uliofanywa Ijumaa.
Wanasiasa wa upinzani wanasema upigaji kura wa digitali, bila ya kutumia karatasi, unatoa fursa ya kufanya udanganyifu.
Tume ya uchaguzi imekiri kuwa kulitokea matatizo kwenye mashini wakati wa kupiga kura, hata hivyo inasema matokeo yatakuwa ya kuaminika. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KESI DHIDI YA MUBARAK YATUPILIWA MBALI

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak. Kesi ya mauaji dhidi yake imetupiliwa mbali na mahakama moja nchini humo.
Mahakama moja nchini Misri imetupilia mbali kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak kutokana na mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa maandamano ya kumng'atua mamlakani.
Aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani wakati wa uongozi wa Mubarak ,Babib al Adly pamoja na maafisa kadhaa pia wameondolewa mashtaka.
Mubarak alihukumiwa miaka miwili iliopita lakini mahakama ya rufaa ikamuondela kifungo cha maisha gerezani.
Mahakama hiyo pia ilimuondolea rais huyo wa zamani mashtaka ya ufisadi.
Bwana Mubarak tayari anahudumia kifungo cha miaka mitatu kutokana na mashtaka ufujaji wa mali ya uma. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...