Tuesday, July 29, 2014

DR. BIRALI AWAONGOZA WATANZANIA SWALA YA IDD

20140729_074656_73ac8.jpg
20140729_074807_771af.jpg
Makamo wa rais Dr. Birali amewaongoza wananchi wa Jiji la Dar es salaam katika swala ya Idd iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja leo asubuhi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mjengwa Blog

ISRAEL: TUTAJILINDA NA HAMAS

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inatakiwa kujiandaa kwa ajili ya mpango wa muda mrefu katika Gaza.
Hata hivyo ameelezea msimamo wake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas. Netanyahu amesema Hamas wanapaswa kusambaratishwa na hilo ndilo lengo la Israel.
‘Tulijua kuwa tungekuwa na siku ngumu, hii ni siku ngumu na ya maumivu kutokana na mashambulizi haya, nguvu na malengo vinatakiwa ili kuendeleza mapambano dhidi ya kundi hilo, anasisitiza Netanyahu.
Wizara ya afya ya Gaza imesema kuwa raia 10 wa palestina wameuawa katika shambulio la makombora yaliyolenga uwanja wa mpira yakitekelezwa na Israel..

Kati ya waliouawa katika shambulio hilo ni watoto saba waliokuwa wakicheza uwanjani hapo ambapo walipigwa na kufa papo hapo.
Hamas imeilaumu Israel kwa shambulio hilo,huku msemaji wa Israel akidai kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa bahati mbaya.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...