Friday, January 10, 2014
MAJIBU YA UBALOZI WA TANZANIA CHINA JUU YA JACKIE CLIFF KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO MACAU/CHINA
Mwezi
December 2013 taarifa zilitoka kwamba kuna binti wa Kitanzania mwenye
umri wa miaka 28 aliekamatwa na dawa za kulevya huko Macao China ambapo
baadhi ya taarifa zilizoripotiwa na Waandishi wa Tanzania zilisema
aliekamatwa ni mrembo ambae amekua akionekana kwenye video kadhaa za
wasanii wa bongofleva (Jackie Cliff).
Thursday, January 09, 2014
SAMAKI MKUBWA AINGIA SEHEMU ZA SIRI ZA BINTI HUKO BUNDA ...!!!
MAISHA ya mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka
12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Bwanza,
Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini baada ya kurukiwa na samaki aina ya
sato, kuingia sehemu ya siri na kukimbilia tumbani.
Tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu iliyopo kandokando ya ziwa hilo.
Akizungumza na Majira, kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka 31, alisema tukio hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji vyake.
Alisema mdogo wake alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.
"Mdogo wangu alifanya jitihada za kumvuta ili aweze
kumtoa lakini alikimbilia tumboni na kuanza kupata maumivu makali, kutokwa na
damu nyingi baada ya kuparazwa na miba ya
mgongo wa samaki
huyo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
GOOGLE YATAJA WATU MAARUFU WA TANZANIA AMBAO PICHA ZA ZILITAFUTWA SANA KWENYE MTANDAO MWAKA 2013
Google trends imetoa list ya majina/maneno ambayo yametafutwa sana kwenye mtandao wa google search kwa mwaka 2013.
Dunia nzima ime-search sana jina la Nelson Mandela likifuatiwa na Paul Walker.
Upande wa Tanzania majina ya watu maarufu yaliyotafutwa sana kwa upande wa picha(image search) ni
Kwa ujumla unaweza kusema jina lililotafutwa sana kwa upande wa image search kwenye google kwa mwaka 2013 ni Wema Sepetu


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
BASI LA MTEI LACHOMWA MOTO NA WANANCHI LIKIWA SAFARINI

Hii ni ajali ambayo imetokea njia Panda ya kwenda Arusha kama unatokea Singida, wakazi wa eneo hilo wamechoma moto basi la Mtei ambapo waandishi wameongea na miongoni mwa mashuhuda na abiria wa ajali hiyo na wametoa haya maelezo hapa chini.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
MAJINA ZAIDI 5,400 YAWANIA UJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

Balozi Ombeni Sefue
********
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema, jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshawasilisha mapendekezo yao ya majina takribani 5, 400, Ikulu.
Kuhusu kutaja baadhi ya majina ambayo asasi hizo zimeyependekeza kwenda Ikulu, Balozi Sefue, alisema ofisi hiyo haina ruhusa ya kufanya hivyo labda asasi zenyewe ziamue kufanya hivyo kupitia vyombo vya habari.
“Jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshaleta majina ya watu 5, 400 zilizoyapendekeza. Mapendekezo yaliyoletwa ni mengi, kwani katika idadi hii, wanaotakiwa ni 2001, hivyo kazi ipo,” alisema na kuongeza:
“Kuhusu majina yaliyopendekezwa, hatuna ruhusa ya kufanya hivyo, labda kwa ridhaa yao wenyewe wanaweza kutangaza kwenye vyombo vya habari. Na sasa kazi tunayoendelea nayo ni uchambuzi wa majina hayo ili tumpelekee Rais, ambaye ndiye atakayejua watakaopaswa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba.”
Subscribe to:
Comments (Atom)










