Thursday, December 19, 2013

MWEKEZAJI WA SHAMBA LA KAPUNGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

rubani wa ndege Andreas Daffee. akipongezana na wakili wake Lweikaza
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewaachia huru watuhumiwa watatu ambao ni Mwekezaji wa Shamba la Kapunga(Kapunga Rice Project) lililopo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya ambao walikuwa wakituhumiwa  kwa mashtaka matatu ambayo ni kula njama,  kumwaga sumu na kuharibu mashamba ekari 557 ya Wananchi.
 
Akisoma hukumu Mhakamani hapo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili watuhumiwa ambao ni Waldeman Veemark ambaye ni meneja wa shamba, Sergei Beacker ambaye ni Afisa Ugani wa kampuni pamoja na rubani wa ndege Andreas Daffee.
 
Mteite alidai kuwa mbali na upande wa mashtaka kuwa na mashahidi 155,ambapo kati yao mashahidi zaidi ya 20 hawakuweza kufika mahakamani huku wengine 9 wakitoa ushahidi wa uongo tofauti na mashtaka yaliyopelekwa.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 19, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


.

TAZAMA PICHA YA NDEGE ILIYOTUA KWA DHARURA KATIKA UWANJA MDOGO WA NDEGE WA ARUSHA BADALA KIA



http://jambotz8.blogspot.com/


Wednesday, December 18, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 18, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
 

..

RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA YAKAMILIKA...!!!


wariobaMwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Warioba. Picha na Maktaba
*********
Dar es Salaam.Hatimaye Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba imekamilisha kazi ya kuboresha rasimu ya kwanza na kupata rasimu ya pili ya Katiba Mpya tayari kwa hatua nyingine.

Taarifa zilizotufikia jana zilieleza kuwa Makamishna na Wajumbe wa Sekretarieti wa tume hiyo, walianza kurejea ofisini juzi na jana, wakitokea Hoteli ya White Sands walikojichimbia tangu Desemba Mosi mwaka huu kukamilisha rasimu hiyo. Awali, Rais Jakaya Kikwete aliiongezea tume hiyo siku 14 zaidi kukamilisha kazi zake. Siku hizo zitakamilika siku 11 kuanzia leo.
Jaji Warioba, Makamu wake Jaji Augustino Ramadhan na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid hawakupatikana kutokana na kilichoelezwa kuwa walikuwa kwenye kikao. Gazeti hili lililazimika kumtafuta Naibu Katibu, Casmil Kyuki ambaye naye alithibitisha taarifa hizo.
“Ni kweli sisi (Wajumbe wa Sekretarieti) tumerejea ofsini jana na wenzetu (Makamishna) walirejea tangu juzi. Kazi zetu tumezikamilisha kilichobaki tunafanya mawasiliano na Mkuu (Rais Jakaya Kikwete), tujue lini tutawasilisha kazi hii,” alieleza Kyuki

Tuesday, December 17, 2013

HILI NI SOMO MAALUM KWA WANAWAKE WANAOTAKA KUOLEWA...!!!

 Hata kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! 
Yes, huu ni ukweli ambao upo wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.
Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke anasubiri kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake. 

Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.  

Je unataka rafiki au mchumba? click neno 2-Chat

Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati Wanawake. 


Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hisia tofauti na kila mwanaume.

Tuyaache hayo, hoja kubwa ya msingi hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.

KIJUE KISIWA CHA ROBBEN JELA AMBAYO MZEE MADIBA ALIISHI KWA MIAKA 27 ILIYOBEBA HISTORIA MZITO DUNIANI


NCHINI Afrika Kusini, hakuna eneo la kivutio cha kitalii linalotembelewa na wageni wengi kama Kisiwa cha Robben. Umaarufu wa eneo hili umekuwa ukiongezeka mwaka mpaka mwaka.
Lakini hakuna shaka kwamba, kiini cha kutembelewa sana kwa kisiwa hiki ni kutoka na kuwa kituo maalumu cha kuwafunga wapigania uhuru wa Afrika Kusini wakati huo, akiwamo Nelson Mandela.

Mandela, Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini, ndiye mhimili wa kivutio cha utalii kwenye jela ya wafungwa wa kisiasa iliyojengwa ndani ya kisiwa hicho.

Kati ya wafungwa wengi wa kisiasa waliowahi kufungwa kwenye jela ya Robben, alikuwamo Govan Mbeki, baba mzazi wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini aliyempokea madaraka Mandela, Thabo Mbeki. Ni Mandela pekee ndiye aliyekaa hapo muda mrefu.

RAIS ZUMA AZINDUA SANAMU YA NELSON MANDELA

zumapix_09bf0.jpg
Pretoria, Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma amezindua sanamu ya shaba ya shujaa wa Afrika, Nelson Mandela kwenye jengo la Muungano lililopo mji wa Pretoria.
Sanamu hiyo yenye urefu wa mita tisa humuonyesha Mandela akitabasamu, huku akiwa ameonyesha ishara ya kukumbatia.


Wakati akizindua sanamu hiyo jana, Rais Zuma alisema kwamba sanamu nyingi za Mandela zinamuonyesha akinyoosha mkono wake mmoja juu kama ishara ya mapambano iliyokuwa ikitumiwa na Chama cha ANC.
Lakini, ishara ya kukumbatia iliyokuwa ikitumika katika sanamu hii ni tofauti, kwasababu inamuonyesha Madiba akikumbatia nchi nzima na watu wake wote bila kujali rangi, itikadi wala tabaka. Zuma aliizindua sanamu hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi ya kiongozi huyo yaliyoshuhudiwa na umati mkubwa watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa nchi tofauti yaliyofanyika katika Kijiji cha Qunu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...