Tuesday, December 17, 2013

LIYUMBA ADAI KUBAMBIKIWA KESI YA KUKUTWA NA SIMU GEREZANI...!!!

Liyumbapix_0473a.jpg
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na simu gerezani, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imfutie shtaka hilo na kumuachia huru kwa madai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kumkomoa.
Liyumba aliyaeleza hayo jana wakati akijitete mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando anayetarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, Januari 15, mwaka na kuzitaka pande zote mbili kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho kama mshtakiwa ana hatia ama la, Desemba 30, mwaka huu.
"Kesi hii imepangwa kwa ajili ya kunikomoa, wakati natumikia kifungo sijawahi kuvunja sheria, kupewa adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote, simu yenye namba 0653004662 siijui nimeiona hapa na kama imesajiliwa ni lazima mhusika atajulikana." alieleza Liyumba.
Alidai kuwa, Julai 2011 alikuwa mfungwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na unapofikishwa huko ni lazima upekuliwe mara tatu kwa kuvuliwa nguo zote.

MBOWE AMNANGA ZITTO KABWE WAZI WAZI, AAPA KUTOVUMILIA USALITI...!!!

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemvaa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kusema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia usaliti wa aina yoyote.  
Akizungumza mjini Mwanza  jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Malimbe, alisema kwa namna yoyote ile hawatamfumbia macho mtu yeyote anayekwenda kinyume cha katiba na taratibu za chama hicho.
  Alisema Chadema ambayo imejengwa kwa damu za Watanzania haiwezi kukubali kuona mtu yeyote anatoboa ‘boti’ yake iendayo kasi katikati ya bahari wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwakani.
Mbali na kumshukia Zitto pia amekirushia kombora Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusema kinatumia mbinu chafu kutaka kuiua Chadema kabla ya mwaka 2015. Alisema kamwe mbinu hizo hazitafanikiwa maana Chadema ipo kwa mpango wa Mungu.

JAMAA AISHI KWENYE HANDAKI MIAKA MINNE...!!!


 
Stori: Makongoro Oging’
DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni kweli.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza samani zote.

“Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.

“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.

“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
“Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea, aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 17, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

Monday, December 16, 2013

"KATIBA MPYA 2014 HAIWEZEKANI" LIPUMBA


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba (pichani) amesema mchakato wa Katiba Mpya una vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais Kikwete alivyoahidi hivyo, kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Bara.
              Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo. Mei mwaka huu, alitoa tamko kama hilo alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya akadai ni janja ya CCM kumwongezea muda Rais.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lipumba alisema kuwa amekuwa akiutafakari kwa kina mchakato wa Katiba Mpya kama unaweza kukamilika mwaka 2014, lakini jibu linalomjia, hakuna.
Alitaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 16, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

ANGALIA MATUKIO YALIYOJILI JANA WAKATI WA MAZISHI YA MZEE MANDELA, QUNU AFRIKA KUSINI




Goodbye to an icon: Nelson Mandela's coffin is slowly lowered into the ground in the hills close to where he grew up at the small, private burial today in Qunu as military salute and mourners watch the poignant moment

Poignant: Nelson Mandela's coffin was carried to his grave and then the flag of the country he loved so ardently was removed and handed to his widow Graca Machel

United in grief: Mandela's widow Graca Michel and his ex-wife Winnie Mandela tearfully comforted one another as they sat next to president Jacob Zuma and Mandela's grandson Mandla as he was laid to rest

Special tribute: The South African air force fly over Mandela's grave in the hills of Qunu where he grew up, which was accompanied by a 21-gun salute


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...