Wednesday, December 11, 2013
Tuesday, December 10, 2013
'BABU SEYA, PAPII LAZIMA WATAACHIWA HURU TU'
NGUZA Mbangu,
mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia
kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema
mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi
karibuni.
Mbangu,
ambaye pia hufahamika kisanii kama Mashine, ambaye hivi sasa ni
mwinjilisti, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumza na gazeti la Uwazi, akisema kuwa kutolewa jela kwa ndugu zake hao, kutawafanya
Watanzania kumsujudia Mungu kupitia tukio hilo.
“Amini
nakuambia, Mungu amenipa maono, Babu Seya na Papii wako huru, watatoka
tu, kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko mbali, ni lazima watatoka kwa
sababu hawana hatia,” alisema Mbangu, ambaye pia alihukumiwa kifungo
cha maisha jela kama mzazi wake, lakini akaachiwa wakati walipokata
rufaa kwa mara ya kwanza mahakamani.
JIONEE PICHA ZAIDI YA 200 ZA IBADA YA KUMUOMBEA MANDELA INAVYOENDELEA IKIWAMO NA MARAIS NA VIONGOZI WALIOWASILI
Sombre occasion: Members of Nelson Mandela's
family take their seats amid heavy rain ahead of his memorial service
at the FNB Stadium in Soweto, near Johannesburg
Respect: Nelson Mandela is shown on a giant
screen inside the stadium as thousands of South Africans and global
dignitaries file into the ground
NORA AFUNGUKA KUHUSU RAY ADAI ALIMTONGOZA. MSIKILIZE HAPA..!!!
Muigizaji wa kike aliyefanya vizuri kupitia kundi la Kaole Sanaa
Group, Nuru Nassoro aka Nora amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na
muigizaji mwenzake Vicent Kigosi aka Ray kwa kuwa aliwahi kumtaka
kimapenzi akamkataa.
Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na
kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo
anapeleka kazi zake.
“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia
wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao.
Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake
sijui kitu gani..” amelalamika Nora.
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.
WINNIE MANDELA NA GRACA MACHEL WAKUTANA MSIBANI, MARAIS ZAIDI YA 90 KUHUDHURIA MAZISHI.... R.I.P MANDELA
Marais
zaidi ya 90 wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Barack Obama wa Marekani
ni miongoni mwa maelfu ya waliojitokeza Johannesburg South Africa
kwenye uwanja wa soka wa FNB leo kumuaga Mzee Mandela anaetarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo December 15 2013.
Serikali
ya Afrika Kusini imeimarisha ulinzi kwa kutumia vikosi vyake vya jeshi
vyenye ulinzi wa hali ya juu ambapo sniper team ni miongoni mwa
wanaohusika na ulinzi kwenye eneo lote la kiwanja anakoagiwa Mzee
Mandela huku helicopter pamoja na ndege za kijeshi zikipita angani mara
kwa mara.
ANGALIA PICHA ZA BIRTHDAY PARTY YA NICK MINAJ, BONGE LA KEKI...!!!
First
lady wa label ya YMCMB Nicki Minaj amesherehekea birthday yake ya
kutimiza miaka 31 na mafanikio ya kujivunia kwenye kazi yake ya muziki
ambapo party ilifanyika huko L.A na Restaurant nzima ilibadilika rangi
yake na kuwa ya pink maalum kwa ajili ya party ya Minaj ambayo
ilihudhuriwa na Lil Twist, Safaree boyfriend wa Nicki Minaj na watu
wengine.
YAFAHAMU MAAJABU 10 YA MSIBA WA MANDELA...!!!
RAIS
wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza
kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na kijeshi
barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake
jijini Johannesburg.
AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia.
Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika
historia, dunia nzima imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila mmoja
akionesha masikitiko yake.
Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo pia yatavunja rekodi ya
mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo
Desemba 15 mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu kumi yanayoambatana na
msiba huo.
AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia.
Subscribe to:
Comments (Atom)






















