Tuesday, January 06, 2015

URUSI KURUHUSU ASKALI KUTOKA NJE

Meli za ulinzi za Urusi 
 
Urusi imeanza kuruhusu askari kutoka nje wenye utalaam ili kuingia katika jeshi lake.
Hata hivyo, wataalam wa Urusi wanasema hatua hiyo haina uhusiano wowote na mgogoro nchini Ukraine.
Rais Vladimir Putin ameidhinisha sheria inayowawezesha raia wa kigeni kufanyakazi angalau kwa miaka mitano katika jeshi la Urusi ili mradi wanajua kuzungumza Kirusi.
Wataalam hao wanatarajiwa zaidi watatoka katika jamhuri za Asia ambazo awali zilikuwa sehemu ya muungano wa nchi za Soviet.
Wageni wa kujitolea, wakiwemo Warusi wamekuwa wakipigana nchini Ukraine. Hata hivyo Urusi imekuwa ikikana kupeleka majeshi yake huko.
Serikali ya Ukraine na nchi za magharibi wanasema Urusi imetuma silaha nzito na askari wenye utaalam wa hali ya juu kuwasaidia watu wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

YANGA KUENDELEZA DOZI KOMBE LA MAPINDUZI...?!

8 (1)
HATUA ya makundi ya kombe la Mapinduzi inatarajia kumalizika leo kwa mechi nne kupigwa viwanja viwili tofauti hapa visiwani Zanzibar.
Mapema majira ya saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, Mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda watachuana vikali na mabingwa wa Zanzibar, KMKM katika mchezo wa mwisho wa kundi B.
Mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Azam fc watahitimisha mechi ya kundi B kwa kuchuana na Mtende, uwanja wa Amaan.
Katika dimba la Mao Dze Tung, Taifa ya Jang’ombe itakuwa kibaruani kuhitimisha mechi ya kundi A dhidi ya Polisi.
Yanga wao watacheza mechi ya mwisho ya makundi kwa kukabiliana na Shaba majira ya saa 2:15 usiku.
Yanga wanaingia katika mechi hii wakiwa tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali kwani mechi mbili za kwanza dhidi ya Taifa ya Jang’ombe na Polisi, zote walishinda mabao 4-0. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SIGARA YAMPONZA KIPA ARSENAL

244D419E00000578-0-image-a-5_1420499963467
Mzee wa fegi, Wojciech Szczesny 
GOLIKIPA wa Arsenal, Wojciech Szczesny ametozwa faini ya paundi laki mbili kwa kosa la kuvuta sigara bafuni baada ya mechi.
.
Bosi wa kipa huyo mwenye miaka 24, Arsene Wenger aligeuka ‘mbogo’ alipomkuta akipiga fegi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton siku ya mwaka mpya.
Szczesny alilazimika kuomba msamaha kwa tabia hiyo, lakini haijulikani kama ataondolewa katika kikosi cha wiki hii kitakachoikabili Stoke kwenye mechi ya ligi kuu England. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

STEVEN GERRARD AIBEBA LIVERPOOL FA

 Steven Gerrard, nahodha wa timu ya Liverpool akishangilia bao na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizoichezea timu hiyo 
 
Steven Gerrard ameonyesha ubora na uongozi na Liverpool itamkosa mchezaji wa aina hii wakati atakapohama Anfield.
Ni Gerrard aliyewainua mara mbili vitini mashabiki wa Liverpool ilipoizamisha AFC Wimbledon mabao 2-1 katika michezo inayoendelea ya Kombe la FA.
Gerrard, akicheza mchezo wake wa kwanza tangu atangaze kuihama Liverpool katika msimu ujao na kwenda kukipiga Marekani, alionyesha pengo atakaloliacha atakapoihama timu yake aliyokulia na kupata mafanikio makubwa.
Nahodha huyo wa Liverpool ambaye atasherehekea miaka 35 katika siku ya mwisho ya Kombe la FA, tarehe 30 mwezi Mei aliiongoza timu hiyo kupata mafanikio na amefanya hivyo mara nyingi wakati timu ilipojikuta katika matatizo.
Gerrard alianza kuichezea Liverpool mwaka 1998. Gerrard amefunga magoli 182 katika michezo 696 aliyoichezea timu ya Liverpool.
Na katika mchezo mwingine Tottenham walitoka sare na Burnley kwa kufungana goli 1-1. Burnley ndio waliokuwa wenyeji wa mchezo huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Monday, January 05, 2015

IPTL YASHUSHA BEI YA UMEME

Sethi Singh

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), imetangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo.

IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme inatarajiwa kushuka zaidi, kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. Marekebisho hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 25 ( Sh bilioni 42.5), yamewezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya marekebisho yaliyokamilika Desemba mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao sasa utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 ya dola ya Marekani (Sh 391) kwa kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 05, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...