Tuesday, January 06, 2015

STEVEN GERRARD AIBEBA LIVERPOOL FA

 Steven Gerrard, nahodha wa timu ya Liverpool akishangilia bao na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizoichezea timu hiyo 
 
Steven Gerrard ameonyesha ubora na uongozi na Liverpool itamkosa mchezaji wa aina hii wakati atakapohama Anfield.
Ni Gerrard aliyewainua mara mbili vitini mashabiki wa Liverpool ilipoizamisha AFC Wimbledon mabao 2-1 katika michezo inayoendelea ya Kombe la FA.
Gerrard, akicheza mchezo wake wa kwanza tangu atangaze kuihama Liverpool katika msimu ujao na kwenda kukipiga Marekani, alionyesha pengo atakaloliacha atakapoihama timu yake aliyokulia na kupata mafanikio makubwa.
Nahodha huyo wa Liverpool ambaye atasherehekea miaka 35 katika siku ya mwisho ya Kombe la FA, tarehe 30 mwezi Mei aliiongoza timu hiyo kupata mafanikio na amefanya hivyo mara nyingi wakati timu ilipojikuta katika matatizo.
Gerrard alianza kuichezea Liverpool mwaka 1998. Gerrard amefunga magoli 182 katika michezo 696 aliyoichezea timu ya Liverpool.
Na katika mchezo mwingine Tottenham walitoka sare na Burnley kwa kufungana goli 1-1. Burnley ndio waliokuwa wenyeji wa mchezo huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Monday, January 05, 2015

IPTL YASHUSHA BEI YA UMEME

Sethi Singh

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), imetangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo.

IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme inatarajiwa kushuka zaidi, kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. Marekebisho hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 25 ( Sh bilioni 42.5), yamewezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya marekebisho yaliyokamilika Desemba mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao sasa utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 ya dola ya Marekani (Sh 391) kwa kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 05, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MIILI 37 YA ABIRIA WA AIR ASIA IMEPATIKANA MPAKA SASA

Vikosi vya uokoaji majini wakitafuta miili ya waliokuwa kwenye ndege iliyoanguka 
 
Shirika la uokoaji nchini Indonesia limesema hivi sasa miili 37 imepatikana kutoka kwenye bahari ya Java ambapo ndege ya Air Asia iliangukia mwishoni mwa juma lililopita.
Helikopta na Meli za kijeshi zimekuwa zikifanya doria katika eneo la bahari hiyo ambapo vitu vinavyoelezwa kuwa mabaki ya ndege vimeonekana.hali ya hewa ya eneo hilo kwa sasa imetengemaa ingawa bado mikondo ya bahari ina nguvu.
Vikosi vya wapiga mbizi wa Indonesia na Urusi vina matumaini ya kupata vifaa vya kurekodia mawasiliano ndani ya ndege, ambavyo vitasaidia kujua sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya kwenda Singapore.
Air Asia ilikuwa imebeba Watu 162 ilipopata ajali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...