Saturday, February 23, 2013
LIGI KUU YA VIDACOM LEO YANGA VS AZAM

Uwanja wa taifa leo mtoto hatumwi sokoni wakati timu mbili zinazotafuta uongozi wa Ligi Kuu zitakapokwaana. Mabingwa wa afrika Mashariki na kati Yanga wataikaribisha Azam katika mchezo utakaovuta hisia za wapenzi wa soka nchini kutokana na zote kuwa juu mwa msimamo wa Ligi kwa kulingana point. Macho pia yatakuwa kwa washambuliaji wanaoongoza kwa ufungaji mpaka sasa, Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye mabao 8 na Kipre Tchetche wa Azam mwenye mabao tisa.
Mwanariadha wa Afrika Kusini mtuhumiwa wa mauaji Oscar Pistorius akubaliwa dhamana.
Mwanariadha
bingwa wa mbio kwa walemavu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi
wake kwa kumpiga risasi Oscar Pistorius amekubaliwa kupewa dhamana.
Wakati
wa kusikiliza maombi ya awali ya dhamana hiyo hapo jana, Hakimu wa
mahakama ya Pretoria ameweka wazi kuwa hakuna aliyemtilia shaka kuwa
atakimbia wala kuwa ana tabia hatarishi.
Pistorius
amekana mashitaka ya mauji, akisema alimpiga risasi Reeva Steenkamp
akidhani ni mvamizi aliyeingia katika nyumba yake.
Kesi
hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 4 mwezi wa 6 mwaka hu.
Pistorius
amekaa katika sero ya polisi mjini Pretoria tangu alipokamatwa mnamo
February 14, 2013.
Friday, February 22, 2013
BREAKING NEWSZZZZZZZZ .... BABA MZAZI WA RAIS MSEVEN AFARIKI DUNIA
Baba wa Rais Museveni afariki
dunia.
Mzee
Amos Kaguta baba mzazi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amefariki dunia
leo
asubuhi huko jijini Kampala Uganda.
Mzee Amos Kaguta amefariki
akiwa na
umri wa miaka 96 na inasemekena alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo
pia
kichwa.East
Africa Radio kwa habari zaidi.
Mzee Amos Kaguta baba mzazi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amefariki dunia leo asubuhi huko jijini Kampala Uganda.
Mzee Amos Kaguta amefariki akiwa na umri wa miaka 96 na inasemekena alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo pia kichwa.East Africa Radio kwa habari zaidi.
Subscribe to:
Comments (Atom)







