Friday, February 22, 2013

LOWASSA ATOA OMBI KWA RAIS KIKWETE



Waziri mkuu aliejiuzulu Mh. Edward Lowassa, amemtaka rais Kikwete aunde tume kuchunguza kilichopelekea matokeo mabaya ya form IV mwaka huu. Amesema tume itasaidia kubaini ni nini chanzo cha tatizo.

Wakati huo huo Mh. Lowassa amemsifu kijana aliyemchora Messi na kusema kijana huyo ni intelligent. Amesifu uwezo wa kijana huyo kufanya hivyo!


Vilevile Mh. Lowassa, ameitaka serikali kuongeza uwekezaji katika elimu kwani amesema tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ndio ya mwisho kwa uwekezaji kwani inawekeza asilimia moja point something ya GDP katika elimu wakati Kenya ni asilimia tano na Rwanda kama sikosei amesema inawekeza mpaka asilimia 7 ya GDP katika elimu na hivyo ametoa wito kwa serikali kuongeza uwekezaji katika elimu.


Mh. Lowassa pia amemsifu Rais Kikwete kwa kufanikiwa katika maeneo mengine kama ujenzi wa barabara, hospitali, zahanati na kwenye maeneo mengine na kumtaka ajielekeze zaidi katika elimu. Mh. Lowassa amerudia kauli yake na kusisitiza kuwa msimamo wake utabaki kuwa ni elimu kwanza na sio kitu kingine.


Miongoni mwa viongozi waliohojiwa ni pamoja na Zitto Kabwe ambaye mbali na kushauri mambo mbalimbali pia amewataka waziri wa elimu na naibu wake pamoja na katibu mkuu wa wizara ya elimu kujiuzulu.


Source: Clouds FM mchana wa leo/jamiiforum

ASKOFU MDEGELA AFICHUA SIRI NZITO YA MAUAJI ZANZIBAR.


Askofu Dkt Mdegela
 

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu
uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na
uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa
vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.

Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa
ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi
hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati
huo.

Mh. Membe kufungua Mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Cooperation), tarehe 24 hadi 25 Februari, 2013


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (Pichani) anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Cooperation), tarehe 24 Februari, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) iliyopo Dar es Salaam.
Mkutano huo pia utahudhuriwa na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdullah anayetarajiwa kuwasili nchini Jumamosi tarehe 23 Februari, 2013 saa 11 kamili jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo mjini Dar es Salaam.
Mkutano huo unatokana na Makubaliano yaliyosainiwa tarehe 14 Oktoba 2009 kati ya nchi hizo mbili mjini Muscat, Oman.
Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Oman katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nishati na Madini, Viwanda na Biashara, Elimu, Afya, Uwekezaji, Utamaduni na Habari.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

RAIS MWAI KIBAKI WA KENYA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI NCHINI


 Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini, wakisiliza taarifa ya pamoja ikisomwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Picha na IKULU

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...