Thursday, April 04, 2013

MAUNO YA WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI

  VIUNO alivyokatika  staa maarufu wa filamu, Jacqueline Wolper viliwachengua ile mbaya watu waliohudhuria harusi ya wasanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu na Idrissa Makupa ‘Kupa’.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Ubungo, jijini Dar baada ya  wasanii kwenda mbele ya ukumbi kwa zamu na kuonyesha uhodari wa kuyarudi mangoma ambapo ilipofika zamu ya Wolper, alionekana kuwazidi wenzake kwa utundu wa kucheza.
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.

RAY ASALIMU AMRI JUU YA FILAMU YAKE INAYO SHUTUMIWA KUUDHALILISHA UKATOLIKI

 
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.

WAJUE WASANII SITA (6) WA BONGO FLEVA WENYE KUHESHIMIKA SANA TANZANIA.

1.LADY JAY DEE
Mwanadada JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi kubwa ya watu walio hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye kuheshimika sana tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya

2.PROF J
Prof J naye hakuwa nyuma katika kutajwa na idadi kubwa,Prof j kama muhasisi mkubwa wa huu muziki wa kizazi kipya anaheshimika sana kutokana na mchango wake mkubwa katika hii gemu bila ya kuwa na sifa mbaya zinazo weza kumchafulia heshima yake
3.FID, Q

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...