Saturday, May 18, 2013

SERIKALI YAAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI VIONGOZI WA WIZARA YA ELIMU WALIOSABABISHA UBOVU WA MATOKEO YA FORM FOUR...!!

Serikali imeahidi kuwajibisha watendaji watakaobainika kwenda kinyume katika uingizaji wa mfumo mpya wa usahihishaji mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, ambao matokeo yake yamefutwa. 


Tume ya Uchunguzi inayotarajiwa kukamilisha maelezo yake hivi karibuni, ilipewa hadidu za rejea ambazo ni kubainisha sababu za matokeo hayo mabaya, kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua. 
Akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kinachosubiriwa sasa, ni maelezo ya kina ya Tume ya Taifa aliyoiunda kuchunguza matokeo hayo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tume hiyo haijakamilisha kazi yake,  lakini muda si mrefu itakuwa imekamilisha na kuwasilisha maelezo ya kina yatakayoipa Serikali majibu kwa maeneo yote.
 
“Tusubiri kidogo, muda si mrefu tutakuwa tumekamilisha kazi …na kama wapo watu waliosababisha jambo hili, wala haitakuwa tatizo hata kidogo kuchukua hatua za kuwawajibisha. Ni dhahiri kwamba suala hili si dogo,”alisema Waziri Mkuu.

Majibu hayo ya Pinda yalitokana na maswali ya Mbunge Sakaya, ambaye alisema uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo kutokana na kubainika kulikuwa na mabadiliko ya upangaji wa alama bila kuandaa wanafunzi, si jambo dogo.

ELIMU YA SHULE ZA MSINGI ITAKUWA NI MIAKA 10 BADALA YA 7...!!

RASIMU ya Sera ya Elimu na Mafunzo nchini inapendekeza kuunganisha elimu ya msingi na sekondari ya kawaida ya sasa ili kuunda elimu-msingi itakayotolewa kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2018, imefahamika. 
Rasimu ya kwanza ya Sera hiyo imeshakamilika na sasa wadau mbalimbali wanatoa mapendekezo yao kuiboresha, kabla ya kupelekwa bungeni ili kutungiwa sheria.
Aidha, mikakati hiyo itakayotekelezwa ni kuhuisha muundo na utaratibu mpya wa elimu na mafunzo kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na mitano anapitia elimu ya awali kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu-msingi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alithibitisha kwa gazeti hili wiki hii mjini hapa kuhusu kukamilika kwa rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2013.
“Ni kweli Sera hiyo imekamilika baada ya kuandaliwa kwa miaka mitatu. Imepita kwa wadau mbalimbali, mashuleni, vyuoni na katika taasisi mbalimbali nchini ambao wametoa maoni yao. “Jumapili (kesho) tunatarajia kuwa waheshimiwa wabunge nao watapata fursa ya kuijadili na kutoa maoni yao katika semina iliyoandaliwa maalumu kwao,” alisema Mulugo katika Viwanja vya Bunge.
Alisema baada ya maoni hao ya wabunge, watapeleka Rasimu hiyo kwa mamlaka husika kwa ajili ya andiko la mwisho kabla ya kupelekwa katika Bunge lijalo ili itungwe sheria kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 18.05.2013

DSC 0261 1a54f

DSC 0262 5766d

SUGU, PROPESA JAY, ROMA MKATOLIKI WAPIGIWA DEBE KUALIKWA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE KUFUATI, BAADA YA MATONYA NA WENGINE KUMTOSA.


 Joseph Mbilinyi aka "Sugu"
 Joseph Haule aka Proffessor Jay"
 R.O.M.A Mkatoliki

 Lady Jay Dee mwenyewe
 K na D wa Maujanja Saplayaz (Kulwa na Dotto)
WAKATI wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wakisubiri kwa hamu kubwa show kali ya Mwanadada Judith Wambura "Lady Jay Dee" ya kuadhimisha kutimiza miaka 13 katika game ya Muziki huo na kutokana na hali ambayo imeendelea kwa baadhi yawasanii mbalimbali waliokuwa wametajwa kushirikiana naye katika show hiyo kujiengua na kutoa sababu kadhaa za kutoshiriki katika Show hiyo (TID, Linah, Barnaba na Matonya)

DIAMOND ATOA SABABU ZA YEYE KUWA KICHECHE......!!!

 KWA mara ya kwanza nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya kueleza sababu za kwa nini ni kiwembe?
Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO

Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.
KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?

Diamond: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?

Diamond: Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.

UWT MBEYA WAMJIA JUU MCHUMBA WA DKT SLAA.


Dkt Slaa akiwa na mchumba  wake Bi Bi.Josephine Mushumbusi Kushoto
Na Esther Macha, Mbeya
UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa
mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri .
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya
Vwawa Mkoani hapa.

Friday, May 17, 2013

WANAFUNZI WA CBE, VETA, UDSM WAJIUZA......!!!

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.

Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

POLISI YAWATIA MBARONI KANGAMOKO ..... RIPOTI KAMILI HII HAPA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na watu hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, Kinondoni Makaburini, Coco Beach na Barabara ya Tunisia.“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamnii.

UN YAWASHAURI WATU KULA WADUDU



Umoja wa Mataifa (UN) umeshauri kula wadudu wengi ili kukabiliana na janga la njaa. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo la UN, kula wadudu wengi kunasaidia kuongeza virutubisho mwilini na pia kupunguza uharibifu wa mazingira.

Tayari watu zaidi ya bilioni mbili duniani wanakula wadudu kama sehemu ya mlo wao. Hata hivyo, UN imekubali kuwa bado kuna watu wengi hasa kutoka nchi zilizoendelea ambao wanaona kinyaa kula wadudu.

UN imesema kuwa kwa sasa wadudu kama manyigu na kombamwiko wanatumika kwa uchache sana kama sehemu ya mlo. Ripoti hiyo imesema kuwa wadudu wapo kila sehemu na wanazaliana kwa wingi sana lakini hawatumiki kama chakula.

Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa wadudu wana virutubisho, hasa protini, mafuta na madini. Wanadai wadudu ni muhimu sana kama chakula hasa kwa watoto ambao hawapati lishe ya kutosha.

Ripoti hiyo imeshauri kuwa sekta ya chakula inaweza kusaidia kwenye kampeni ya kula wadudu kwa kujumuisha recipes mpya za wadudu katika vyakula vyao na kuongeza wadudu kama menu kwenye mahoteli. 

Uko tayari kula wadudu kama kombamwiko (mdudu wa jamii ya memde) kama sehemu ya mlo wako?

CD ZA UAMSHO NA ZILE ZA SHEIKH ILUNGA ZAPIGWA MARUFUKU....!!



Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamu  wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi CD  zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.
 

Agizo hilo lilitolewa na OCD  wa  zamani Murtad MKADAM ambae kwa  sasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif. 

Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam.
 

OCD alibainisha kuwa mpaka sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha  na  kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani serikali ina mkono mrefu.
 ...

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.

TUHUMA: MAWAZIRI KUUZA DAWA ZA KULEVYA

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola
  Mbunge sasa 'asakwa' kiana
  Pinda akwepa, awasafisha
Serikali imembana Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, kwa kumtaka awasilishe ushahidi kuthibitisha kuwa baadhi ya mawaziri wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mbunge mmoja kuitaka serikali itoe kauli kutokana na madai kwamba mawaziri wake wanajihusisha na biashara hiyo haramu.

Mbunge wa Tumbe (CUF), Rashid Ally Abdallah, alitaka kauli ya serikali jana alipouliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema kuwa mbunge aliyetoa tuhuma hizo apeleke ushahidi, ili upelekwe kwa Rais.

Katika swali lake Abdallah, alisema kuwa Lugola alitoa kauli akisema wapo baadhi ya mawaziri wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, licha ya wabunge hao kulindwa na ibara ya 100 ya katiba.

HUU NDIO WARAKA WA MASHITAKA YANAYO MKABILI MSANII LADY JAYDEE MASHTAKA YALIYOFUNGULIWA NA JOSEHP KUSAGA NA RUGE MTAHABA


Mwanamuziki Judith Wambura, amepigwa stop na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni kuongelea lolote kuhusiana na ugomvi wake na viongozi wa Clouds Media Group, nje ya mahakama mpaka hapo kesi yake ya msingi dhidi ya viongozi hao ambao ni wadau wa burudani itakapomalizika.

Katika status yake aliyoiandika muda mfupi tu kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lady Jaydee ambaye siku za karibuni amekuwa maarufu kwa jina la Anaconda amesema:

"Nadhani baada ya hii, maswali yatapungua kama sio kuisha kabisa...Nafahamu kila mtu anasoma kwa wakati wake pengine hamkuona sababu nilizoelezea kwanini sijatoa waraka mwingine Tar 15 kama nilivyo ahidi.

Sababu ni kuwa mahakama imesema nisizungumzie hilo swala kwasasa, ambapo kesi bado iko mahakamani...Mpaka nitakapopewa ruhusa ya kuzungumza au kutozungumza tena".
-
Mdimuz

MOVIE ALIYOFANYA MAMA KANUMBA KUTOKA KESHO MITAANI, HAWA NDO WAHUSIKA WAKUU

fffffffffffffffffffffffffffffff
Movie titled “Without Daddy” ambayo imepata kick kutokana na Mama Kanumba kuwa ndani yake, kesho itakuwa mitaani. Watu wengi wana hamu kubwa ya kuona jinsi gani mama Kanumba anauwezo kiasi gani kwenye ishu za kuigiza. Basi usikose kuikamata copy yako kesho na uangalie jinsi gani mama Kanumba kafanya mambo humu ndani. Kweli alimpa kipaji mwanae au ni vingine?

HUU NDIO WARAKA WA 'ANTIVIRUS' KWENDA KWA RUGE NA KUSAGA!! USOME HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5XHEZ5q85-oyxw_UcRunmglJKxUKAuUy-5b4mEa-6uNsPv06vU8iPGScZjMT2LvGytaQjZa33m5EEesulepmqHh2kcbWXXTtQc9hLq1KCfyiG4wBvq7hmj9A4A9AyS_vrJbtnwvM8u2k2/s1600/Anti+virus.jpgANTiVIRUS DAWA YA Virus WA Hiphop in Tanzania

WARAKA NAMBA 1(ZIPO 88) KILA WIKI UTAPATA WARAKA MMOJA

Ni wazi na dhahiri kabisa kesi iliofunguliwa mahakamani dhidi ya Lady JayDee haina maana yoyote isipokuwa ni hofu ya mafisadi wa muziki nchini (Kusaga na Ruge) kwa kuwa waraka wa pili ulikuwa utoke tar 15 may na mwingine tar 17 may mwaka huu wa 2013.

Hapa la kujiuliza ni juu ya interview ya Rugen a kinachoendelea sasa,eti suala limefika mahakamani,kweli Kusaga na Ruge mmeweza kuthibitisha nyie ni mafisadi na mnamuaibisha Rais Kikwete ambaye nina uhakika anajua kuwa nyie ndio kikwazo kikubwa na hata Bungeni alishawahi kuzungumza kuwa alitoa studio na pango kumbe tatizo sio hilo,tujiulize wote kuna nini wanachoficha hadi kumtafutia kesi raia mwema asie na hatia?

Tena anaejitafutia rizki ambayo wao wanapigana nayo kwa kumkandamiza?
Huku wakitumia mabavu wakilindwa na baadhi ya viongozi wa serikali na waandishi ambao majina yao mtayapata kupitia nyaraka zinazokuja (zipo 88) na huu ndio wa kwanza.
Nimesikitika sana na njia pekee ya kuufahamisha umma juu ya ufisadi huu wa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga ni kuyaanika yote ambayo jamii na Viongozi wa Serikali kama mlikuwa hamjui sasa ndio wakati muafaka wa kuwajua watu hawa ambao kila kukicha ni kuimarisha ufisadi wao na kujipendekeza kwa Viongozi sambamba na watoto wao (mtajua mpaka majina yao)

Tukio la bomu latua UN


Tukio la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt.
Askofu Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.
Bomu hilo lilirushwa katika kanisa hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu na
kujeruhi zaidi ya 50.

Wakati wa shambulizi hilo, Askofu Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu walionusurika.

LINAH, BARNABA KUTUPIWA VILAGO THT?

Msanii Linah 
Barnaba
Na  Andrew Chale
KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’  huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu. 
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake. 
Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.
“Juzi Lina,haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushauri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.

T.I.D NAE AJITOA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE, HIKI NDO ALICHOKISEMA.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoEWu1lllJh5WkHOymJ8BTvguRy_0NBr6aFmlmkY-F3UY9hJJWH3rLa9WK6OmqIBG3xsGAvlak8T4GhVKY_V-g83fwaedgdypfPbtJtmuhGikj0cm2wa5YA2f4nR3-UO5OdmZelF4GKa1p/s400/DSC05754.JPGShow ya miaka 13 katika muziki ya Lady Jaydee inazidi kupata pigo baada ya TID kuwa msanii mwingine latest kujitoa kwenye show hiyo.

401187_10150536949328749_793704636_n
Moja ya sababu anayosema TID ni kuwa ana mkataba mwingine wa show unaolipa zaidi.. Sababu ya pili ni kuwa hataki kuwa katikati ya ugomvi wowote.
Hivi ndivyo alivyoandika TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Three reason why i can’t do lady JIDE SHOW ………….No.1 I have better contract pays me better than.No.2 I really don’t want to be between anybody’s conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari…No.3 nataka kuoa muda wangu ndo huu ……………kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been thru same shit.”
Tayari Linah, Barnaba na Matonya wamejitoa kutumbuiza kwenye show hiyo.

MWANAMAMA HUYU AMEKUWA GUMZO KATIKA MJI WA MTWARA MTIZAME HAPA CHINI



 Pikipiki ilirukiwa fasta na Mwana mama huyu, wasio mfahamu wengi walimshangaa, alivaa Kofia ngumu kisha akapachika pochi yake anapotaka na kisha akaiwasha. Huu ni usafiri wake anaoumiliki na huutumia mara zote katika mishe mishe zake.

Safari ikaanza na gia ziilingizwa mama huyu ni maarufu sana Mjini Mtwara
  
Nilikuwa naona vumbi tu linatimka na masihara niliyodhani anafanya kumbe ndio alikuwa akiondoka na huo ndio usafiri wake.Picha na Father Kidevu

VUNJA MBAVU ZA WAZIRI MAGUFULI BUNGENI DODOMA


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
Na Mohammed Kuyunga
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ndiye waziri namba moja hadi sasa kwa kulivunja mbavu Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma kutokana na vichekesho vyake wakati alipokuwa akijibu hoja za wabunge mbalimbali hivi karibuni.

Magufuli ambaye wengi humuita ‘Jembe’ kutokana na uchapa kazi wake, alikuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake na kuomba kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 1.22 kwa mwaka wa fedha 2013/14.

Mheshimiwa huyo alimudu kuwafanya waheshimiwa wacheke sana huku ujumbe ukifika tofauti na mawaziri wengine waliopita ambao hotuba zao zinadaiwa kuwa zilijaa ushawishi wa usingizi.

KIONGOZI WA CHADEMA ATUHUMIWA KUMLAZIMISHA KUTOA MIMBA

"Fridah Kerubo mwanafunzi wa chuo cha MDU Rohtaki India anayesoma masters ya Sheria yupo tayari kutoa ushuhuda jinsi Mtanzania Ben Saanane alivyompa Mimba na kisha baadae kumshawishi kuitoa la sivyo angemuonyesha kila rangi na kisha baadae kwenda uinereza.
Pia yupo Sally Mukhanji ambaye yupo Tanzania sasa hivi amemaliza kutupa ushuhuda jinsi Ben maarufu kama HR yaani Hit and Runalivyokua akifanya biashara ya Dola Fake,na Euro akiwa New Delh India. Picha hiyo ya wadada wa pili ambaye alipiga na Ben ambaye mkono ndiyo unaonekana ameitoa pamoja na nyingine nitazileta soon. Huyu anajua mengi yaliyofichwa . Sasa kama chadema imejaza watu kama akina Lema aliyebaka, Mnyika aliyekutwa na mwanafunzi quality plaza na mbowe aliyempa mimba mbunge wa viti maalumu kama alivyoripoti kamaradi Mtela Mwampamba unategemea nini. Hawa Wakenya wanalalamika na nitashangaa kama kuna mwanaume wa kitanzania atafurahi kuchafuliwa image yake kama ben alivyoharibu sifa ya wanaume wa kitanzania.Turekebishe tabia za wanasiasa wetu. Matusi ya vijana wa Chadema hayanisumbui maana kama mnapanga kuteka watu hakuna msiloshindwa
KWA HISANI YA Eddah Kishimba

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17.05.2013

DSC 0230 cd07d

DSC 0236 d1506

MBUNGE MSIGWA AMTAKA KINANA KWENDA MAHAKAMANI KESHO



Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka  wafanyabiashara  ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa  kuendelea  kufanya kazi katika  eneo la Mashine  tatu  bila  kufanya  vurugu  zozote kwa  wale wanaozuia kufanya  hivyo. 
Akizungumzia  suala la Machinga  kuendelea  kunyanyasika  mbunge Msigwa amesema  kuwa tayari suala  hilo ameanza  kulipigania bungeni  kwa waziri  mwenye dhamana  hivyo kamwe  machinga  Iringa  wasikubali  kunyanyasika . 
Aidha mbunge  huyo amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Bw  Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho. 
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli kama  hata  kuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hiliMbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima. 
Kwani  alisema  kuwa  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote .
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo jioni hii katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani.

MSANII WA CAMP MULLA ALIYEWAHI PIGA CHAFU ATIMULIWA NDANI YA KUNDI HILO


 

Habari zilizosambaa katika mitaa ya area code +254 zinadai kuwa kundi la hip hop lenye mafanikio makubwa nchini Kenya, Camp Mulla limempiga chini first lady na lead singer wa kundi hilo, Miss Karun  kutokana  na  skendo  zinazomkabili
Kwa mujibu wa maneno ya mtaani  inasemekana nafasi ya Miss Karun itachukuliwa na mrembo mwingine aitwaye Tiri, ambaye ni mpenzi wa member na producer wa kundi hilo K’cous
Miss Karun
Siku chache zilizopita kulizuka uvumi wa uwezekano wa members wa kundi hilo kuendelea na solo projects kwa kila mmoja wao ifikapo mwezi June 2013, kitu ambacho kinafanya tetesi za Miss Karun kuondolewa kundini kuchukuliwa kama dalili za kuvunjika kwa kundi hilo.
Camp Mulla wanategemea kupanda kwenye jukwaa moja na Snoop Lion katika concert ya MTV all stars Kwa Zulu-Natal hivi karibuni nchini Africa Kusini, show ambayo watampandisha mrithi wa Miss Karun kwa mara ya kwanza.

Thursday, May 16, 2013

BAADA YA FERGIE NA SCHOLES - DAVID BECKHAM NAE ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU


Kustaafu ndio habari iliyoshika hatamu nchini Uingereza hiv sasa - wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hiimchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa EnglandDAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga. Beckham, 38, ameisadia Paris Saint-Germain kubeba kombe la  Ligue 1 kwa mara ya kwanza ndani miaka 19 mwishoni mwa wiki hii.
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huuA.
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”
Becks alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer. 

CCM YAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI


   Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana jana Mjini Dodoma imeipongeza serikali kwa hatua inayoendelea kuchukua katika kuchunguza chanzo cha tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea Kanisani Jijini Arusha.
Bomu hilo lilirushwa Mei Tano mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Romani Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olisiti na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE ameeleza kuwa taarifa hiyo ya serikali iliwasilishwa jana katika kikao hicho na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dokta EMMANUEL NCHIMBI .
Kufuatia tukio hilo, Kamati Kuu imelaani na imeitaka serikali kuharakisha uchunguzi pamoja na kuongeza kasi ya uchunguzi wa suala hilo sanjari na kutafuta mzizi wa matukio hayo pamoja na kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa tukio hilo.

AUNT LULU AAMUA KUACHANA NA MASHOGA....!!


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amepigwa ‘stop’ kutembea na marafiki wanaodaiwa kuwa ni wanaume wenye vitendo vya kike ‘Kuku Watamu’.

Akizungumza na mwandishi  wetu, Aunty Lulu alisema baada ya kuandamwa na maneno juu ukaribu wake na wanaume hao, mama yake mzazi na mpenzi wake wa sasa ambaye hakutaka kumtaja, wamemzuia ‘kumpiga stop’ kumuona na watu hao.
  
“Sasa hivi ndugu zangu ndiyo wamekuwa marafiki zangu, sitembei kabisa na kuku watamu. Siwezi kumuudhi mume wangu mtarajiwa, mama na hata ndugu wengine, nimeamua kuachana nao,” alisema Aunty Lulu ambaye pia ni mtangazaji ‘deiwaka’.

KOCHA WA TAIFA STAR KIM ATAJA TIMU YAKUIKABILI MORROCO

kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ameongezewa mkataba wa miaka miwili, leo ametaja kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco mwezi ujao kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani.


Katika kikosi hicho, kocha huyo Mdenmark amemuorodhesha kipa wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’ pamoja na makipa wengine watatu, Juma Kaseja wa Simba SC, Mwadini Ally na Aishi Manula wa Azam.

Upande wa mabeki amewaita Erasto Nyoni, Aggrey Morris wa Azam, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC, Shomary Kapombe wa Simba SC na Yahya Mudathir wa Azam.

Kwa viungo, Poulsen amewaita Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa wa Simba SC, Simon Msuva, Frank Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’ wa Yanga SC, Salum Abubakar, Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Azam FC na washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC, John Bocco wa Azam FC, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na Zahor Pazi wa JKT Ruvu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...