Ukweli
ni kuwa watu wawili wanapoamua kwa dhati
kuwa katika mahusiano ni kwamba wanakuwa tayari katika akili zao wamejenga
matarajio au matumaini ya kunufaika na uhusiano husika, hata kama hawawezi
ambiana moja kwa moja kuwa “ aisee, mie kuwa na wewe nataraji moja , mbili,
tatu….”.
Kunapokuwepo
na upendo, basi pia kunaleta majukumu, ambapo bila ya kutimizwa kwa majukumu
yanayotarajiwa kutimizwa, maana halisi ya mahusiano bora inapotea.
Hii
si tuu kwa mahusiano ya kimapenzi, bali hata dini zinatufundisha kuwa Mungu
anatupenda, na katika hilo, tunajukumu la kutii amri zake, na kwamba tusipotii
amri zake, tunakuwa tumeharibu maana nzima ya upendo wake, kwani tutajikuta
tumeingia motoni/jehanamu (Kinyume cha upendo).
Hata
katika familia, tumesikia mzazi pamoja na upendo alioonyesha kwa mtoto wake
toka yupo tumboni mpaka mtoto ameweza kujitegemea, endapo mtoto husika
akashindwa kumjali ( hili ndio jukumu linalokuja na upendo wa mzazi), basi
unaweza sikia mzazi huyo akitoa ‘laana’ au ‘akamwachia radhi’ mtoto wake
mwenyewe wa kumzaa.
Ni
wazi kuwa mara nyingi majukumu yanayoletwa na upendo huwa hayaelezwi wazi wazi,
hata hivyo katika mahusiano, mambo yafuatayo yanaweza kuwa sehemu ya matarajio
ambayo wapenzi wanaweza kuwa makini ili
waweze kuwapendeza wenzao. Kwa maana nyingine ni kuwa yafuatayo, ndio maeneo
ambayo mtu aliye kwenye mahusiano ni muhimu ‘acheze’ vema ili kulinda
mahusiano/penzi:-
Fedha: Katika swala la fedha, jambo kubwa
linalojitokeza ni namna ya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya fedha. Ni muhimu kuweka mikakati ya pamoja kwa mambo
ya msingi kimaisha , na kila mmoja kutilia maanani mipango hiyo, kabla ya kuamua
kutumia kipato chake kwa mambo ambayo pengine hayapo nje ya mipango ya kifedha
ya wawili nyie kama wapenzi. Bila shaka,
kuendana na aina yenu ya kipato, aina yenu ya maisha, kama wapenzi mtakuwa na
kiwango fulani cha fedha ambacho si busara mmoja wenu kuamua kutumia bila
kumtaarifu mwenzake , hata kama matumizi husika ni muhimu sana, na haijalishi
nani kazitafuta fedha husika.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz