Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira
akizungumza kwenye mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia
ni Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) Tundu Lissu na katikati ni
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira akiwakilisha CCM,
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa CUF, Profesa
Ibrahim Lipumba, jana walitoana jasho katika mdahalo wa Katiba
ulioandaliwa na East African Business and Media Institute.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao
500, ulikuwa na mada inayosema: ‘Nani anakwamisha Upatikanaji wa Katiba
Mpya.’ Kila upande ulitumia fursa hiyo kutupa shutuma kwa mwingine huku
jazba na kelele vikitawala miongoni mwa waliohudhuria.
Hata hivyo, suala la muundano wa serikali ndiyo
uliochukua nafasi kubwa katika mdahalo huo huku Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ukiishutumu Serikali ya CCM kuwa ndiyo kikwazo cha
upatikanaji wa Katiba Mpya nayo ikitupa mpira huo kwa Ukawa kwa kitendo
chake cha kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz