Moja ya ndege zinazo milikiwa na shirika na ndege la Misri. | NYOKA aina ya Cobra amesababisha kizaza kwenye ndege na kuilazimisha kukatisha safari yake na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Hurghada nchini Misri, auliwa baada ya kumjeruhi abiria . | |
| Nyoka huyo alizua mtafaruku huo baada ya kutoka katika mfuko alipokuwa amehifadhiwa na kumjeruhi abiria mmoja raia wa Jordan aliekuwa amekaa karibu na mfuko uliokuwa amehifadhiwa nyoka huyo. Abiria walianza kumshambulia wakijaribu kumuua kwa kumpiga na viatu na hatimae kufanikiwa kumuua, abiria aliejeruhiwa alipatiwa huduma ya kwanza, na kuhamishiwa hospitalini kwa matibabu zaidi na kuwekwa chini ya uangalizi kwa masaa 24, hali iliopekea kukatisha safari yake. Uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kwamba, mmoja wa abiria alimficha nyoka huyo kwenye mkoba na alifanikiwa kupita katika vizuizi na kuingia na nyoka huyo kwenye ndege. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz | ||
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mwajuma Hamisi, mkazi wa Yombo Vituka kwa kosa la kukutwa na ngozi mbili za chui kinyume cha sheria, zenye thamani ya sh milioni 11.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema mwanamke huyo alinaswa Januari 18, mwaka huu katika eneo la Yombo Vituka, Wilaya ya Temeke.
Kova alisema mwanamke huyo alinaswa baada ya Ofisa Mhifadhi Wanyamapori mkazi wa Ukonga, kutoa taarifa kituoni hapo kwamba kuna mwananchi anauza ngozi za chui.
Alisema askari walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na walipompekua chumbani kwake, walimkuta na nyara hizo za serikali.
Wakati huo huo, jeshi hilo limesema limemuua jambazi sugu la uhalifu wa kutumia silaha katika majibizano ya risasi na polisi.
Alisema awali polisi waliweka mtego ili kuyanasa majambazi hayo Januari 22 baada ya kufanya tukio la uporaji wa sh milioni 29 kwa mfanyabiashara wa Mtaa wa Kariakoo, anayejulikana kwa jina la Shanys Abdalla, mkazi wa Mbezi.





















