Wanajeshi na polisi wa Ufilipino
wamepelekwa katika miji ilioathirika na kimbunga kikali kuwahi kuipiga
nchi hiyo ili kudhibiti wizi wa mali unaohatarisha juhudi za kutoa
misaada ya kibinaadamu kwa waathirika.
Zaidi ya watu 10,000 wanahofiwa
kufariki kutokana na kimbunga hicho kwa jina Haiyan kilichopiga kwa
mawimbi mazito na upepo mkali na kusababisha athari kubwa nchini
Ufilipino siku ya Ijumaa, huku mji wa Tacloban ukiwa moja ya miji
ilioathirika pakubwa.
Waokoaji kwa sasa wanajaribu kupeleka
misaada ya chakula na malazi kwa waathirika wa kimbunga hicho katika mji
huo ulio na idadi ya watu 220,000.
Hata hivyo hatua hiyo iliendeshwa kwa
changamoto kubwa kutokana na wizi uliokuwa ukiendelea. Waporaji
walivunja maduka pamoja na kuvamia gari la misaada la msalaba mwekundu
na kuchukua vile vilivyokuwemo ndani.
Baadhi ya waathiriwa ambao ni wafanyabiashara wadogo pia wameripoti kuibiwa kwa televisheni, na mashini za kufulia nguo.
Kulingana na msemaji wa wizara ya ulinzi wa raia nchini humo, Reynaldo Balido, kurejesha usalama na hai ya utulivu katika mji huo wa Tacloban, ni moja ya mambo wanayoyapa kipaumbele.