Friday, September 20, 2013

KINANA ATAKA WALIMU WATATULIWE KERO ZAO HARAKA

2
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia waimbaji wa kwaya mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nyashimo Wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu, Ndugu Abdulrahman Kinana amemaliza ziara yake kwenye mkoa huo ambapo amekagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wenyeviti wa mashina pamoja na wanachama wa CCM ili kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali moani humo, Kinana anaaza Ziara ya siku sita katika mkoa wa Mara. Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo uliofanyika mjini Lamadi Busega Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasiapamoja na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili kumaliza tatizo la malimbikizo hayo, Kinana amesema kama watendaji hao wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya Kikwete ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu, Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus Kamani. (PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LAMADI SIMIYU) 
 1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakifurahia ngoma za akina mama walipowasili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. 9

KUDHIHIRISHA KUWA YUPO NJE KWA DHAMANA HIZI NDIZO PICHA ALIZOZISAMBAZA AGNES MASOGANGE MTANDAONI




MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 20, 2013

DSC 0032 8b966
DSC 0033 c2442

MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO LA KIISILAMU

mrembo 25c93
Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.


Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku ya Jumatano.
Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CUF, CHADEMA NA NCCR HAPO JUMAMOSI



Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA siku ya Jumamosi yaliyokuwa yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani na Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali ...

Taarifa  iliyotolewa  na kamanda Kova  kupitia  ITV   imeeleza  kuwa  Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

Source: ITV HABARI SAA 2 usiku

MILIONI 58 ZAPATIKANA mechi SIMBA SC, MGAMBO TANGA

Boniface-Wambura1 655d3
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Simba SC na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza Sh. 58,365,000.

Watazamaji 10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh.
4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,641,954.10.

Wakati huo huo; Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka huu.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni. Chanzo: TFF

HAKIMU ACHOMWA KISU MAHAKAMANI

hakimu_1e5b7.jpg
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.


Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.
Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.

Thursday, September 19, 2013

ICC YATAKA MAREKANI IMKAMATE RAIS BASHIR

al-bashir_bcdb9.jpg
Siku mbili baada ya Rais wa Sudan kuiomba Marekani kumpa Visa ya kusafiri nchini humo kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, wito umetolewa kwa taifa hilo kumkamata Bashir na kumkamabidhi kwa mahakama ya ICC.
Mkutano huo utafanyika wiki ijayo.
Ombi hilo limetolewa na ICC kwa Marekani na kuitaka impe Visa Bashir na kisha kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo pindi tu atakapotua nchini humo.
Bashir anatakikana na mahakama ya ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na pia kuamuru mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur.
Marekani ilisema kuwa ilipokea ombi la Bashir kutaka Visa na kulitaja ombi hilo kama la kuudhi na kejeli kubwa kwa taifa hilo. Ilimtaka Bashir kwanza kujikabidhi kwa mahakamya ICC kabla ya kutaka kuingia Marekani.
Hata hivyo Marekani sio mwanachama wa mahakama ya ICC na kwa hivyo , kisheria sio lazima itimize matakwa ya mahakama hiyo juu ya Bashir.
Marekani imekuwa katika msitari wa mbele kutaka Bashir akamatwe kwa madai ya uhalifu dhidi yake ili akabiliwa na sheria za kimataifa
Shirika la habari la Reuters lilisema kua mahakama imeshauri Marekani kumkamata Bashir na kumkabidhi kwa ICC ikiwa ataingia nchini humo.
Vibali viwili vya kumkamata Bashir vilitolewa mwaka 2009 na 2010 kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Sudan imepuuza hatua ya ICC kumtaka Bashir kwa makosa ya Darfur wakisema kuwa madai hayo yameongezwa chumvi, na nchi hiyo imekataa kuitambua mahakama hiyo ikisema kuwa ni sehemu ya njama ya nchi za magharibi dhidi ya Afrika.

TANZANIA YAMKATAA BALOZI WA UJERUMANI

Balozi Margit Hellwig-Boette 
******
Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini.
Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette alikuwa amemaliza muda wake nchini Kenya na alitakiwa kuja kuiwakilisha nchi yake Tanzania.
Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na Gazeti la Standard la Kenya akieleza kuwa anajipanga kurudi kwao baada ya kukataliwa na Serikali ya Tanzania.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ndio wanaoshughulika na hayo mambo, waulizeni.”

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema wizara yake haijapata taarifa za kukataliwa kwa balozi huyo.
“Suala hilo linahusu ofisi ya Rais, mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa na hata kama ingekuwapo hiyo taarifa siyo ya `public’.
“Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.
“Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine,” alisema Mkumbwa.
Alikariri Kifungu cha Nne cha Azimio la Vienna ambacho kinaruhusu nchi kukataa balozi wa nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
“Nchi inayopeleka balozi katika nchi nyingine inatakiwa kutoa jina mapema kwa nchi nyingine. Hata hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa kumkubali au kukataa uteuzi,” kinaelekeza kifungu hicho.
MWANANCHI

RAIS KIKWETE AWASHUKIA WANASIASA


 
Rais Jakaya Kikwete
 
*Asema hatawatetea wauza ‘unga’
*Ashangazwa na kiwango cha uongo

RAIS Jakaya Kikwete, amesema anashangazwa na kiwango cha uongo cha baadhi ya wanasiasa ambao hakuwataja majina, kuwa wamekuwa wakizusha madai kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
Alisema bado anaendelea kuamini mchakato wa Katiba mpya utafikia mwisho wake mwaka 2014 na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, chini ya Katiba mpya.

Alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera za serikali ama hata kumpinga yeye binafsi, bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.

Rais Kikwete, aliyasema hayo juzi, mjini San Rafael, California, nchini Marekani, wakati alipokutana na kuzungumza na jumuia ya Watanzania waishio katika Jimbo la California.

Katika hotuba yake, ambayo alizungumzia mambo mbalimbali, Rais Kikwete aligusia mjadala wa karibuni bungeni kuhusu mchakato wa Katiba mpya na kusema kuwa alishangazwa na madai kuwa yeye kama Rais, hakuongozwa na mapendekezo ya wadau wakati anateua Tume ya Katiba.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 19, 2013

DSC 0013 2232e
DSC 0014 fd5f3

MATOKEO KAMILI LIGI KUU TANZANIA

1111 1e313
YANGA 1 - 1 Prisons,
SIMBA 6 - 0 Mgambo
Kagera 2 - 1 JKT Oljoro (HM)
Azam 1 - 1 Ashanti
Coastal 1 - 1 Rhino
Mtibwa 0 - 0 MBEYA City
Ruvu Shooting 1 vs 0 JKT Ruvu. Chanzo: Shaffihdauda

ANGALIA VIDEO YA LINAH AKIFUNGUKA JUU YA PENZI LAKE NA AMINI




Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa ni mjasiriamali pia Anasteria Sanga Linah au muite Ndege Mnana amefunguka kuwa producer wa studio ya Bhitz Pancho Latino ndiye mwenye siri nzito ya penzi lake na msanii mwenzake Amini ambaye kwasasa penzi lao limekuwa stori ya kale baada ya kuachana. Linah amesema tokea wanaanza mapenzi yao Pancho ndiye alikuwa mtu pekee anayejua mambo mengi kuwahusu wao na jinsi walivyotumbukia katika penzi ambalo anasema yeye binafsi ndiye hasa alikuwa akimpenda Amini kupita kiasi japo baadaye akagundua kuwa hata mwenzake naye anamzimika na hivyo penzi likawa linasonga.

"Yaani we muulize Pancho yule ndio ana siri kubwa sana ya penzi langu na Amini,yaani jamani nilimpenda sana Amini mpaka nikakubali kuingia kwenye mapenzi na nilimpenda hasa kutoka moyoni,kuna vitu vingi nyuma yake ambavyo Pancho anajua",alisema Linah.

Msanii huyo mwenye sauti tamu kiasi cha kupachikwa jina la Ndege Mnana na msanii mkongwe Patricia Hillary ameendelea kufunguka kuwa wakati ameangukia katika penzi la Amini alikuwa anawachomolea wanaume wengi waliokuwa wanamtokea tena wenye pesa zao na wengine ni watu wazito lakini aliamua kutoka moyoni kwa dhati kuwa na Amini kwahiyo akawa anamtunzia heshima yake.

RIPOTI YA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNES MASOGANGE NA MELISA HUKO AFRIKA KUSINI..!!

WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.
 
Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
 
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
 
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

NAPE AWACHONGANISHA CHADEMA NA WAKULIMA WA PAMBA

blog_756b7.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya Sabasaba. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira.
-Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema.
-Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.

Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu. Alisema hoja kuwa ambayo imewakera na kuwasumbua Chadema ni hatua zinazochukuliwa hivi sasa kwa pamoja kati ya Serikali ya CCM na Serikali ya China ambayo hivi sasa inaelekea kuzaa matunda ya kutoa mwanya wa ajira zaidi ya elfu- 25 viwandani.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...