Wednesday, August 21, 2013

MADIWANI BUKOBA: TUKO TAYARI KUHAMIA CHADEMA....!!!

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofukuzwa katika Manispaa ya Bukoba, wamesema wako tayari kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kama chama chao kitaendelea na msimamo wa kuwafukuza. Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, mmoja wa madiwani hao (jina na kata yake tumevihifadhi), alisema wako tayari kuhamia Chadema muda wowote kama hawatarudishiwa uanachama wao.

Alisema, madiwani wote waliofukuzwa wana msimamo mmoja, ambapo wanasubiri vikao vya Kamati Kuu ya CC ili wajue hatima yao, lakini vikishindwa kuwarudisha kwenye chama, watahamia Chadema ili kuendeleza harakati zao walizozianzisha.

Alisema, wanachokifanya wao ni kutetea maslahi ya taifa na wananchi waliowapigia kura na si kulinda biashara za watu binafsi, hata kama wanaungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM.

Msimamo huo wa madiwani umekuja siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuwakaribisha madiwani hao katika chama chake na kusema wako tayari kuwafundisha siasa za mageuzi.

GODBLESS LEMA AUGUA GHAFLA, KESI YAKE YAHAIRISHWA




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha jana imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa.

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Hawa Mguruta, anayesikiliza shauri hilo kuwa Lema anaumwa na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya AICC tangu Agosti 14 hadi 19, mwaka huu aliporuhusiwa kutoka hospitali, hivyo ametakiwa apumzike kwa muda wa siku 10 kuanzia Agosti 19, mwaka huu.

Wakili Kimomogoro aliomba shauri hilo liahirishwe hadi siku nyingine, ombi lililokubaliwa na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1 na 2 mwaka huu, ambapo mashahidi tisa wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

DIAMOND NAE ATAJWA SAKATA LA UNGA....!!!



*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange

KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.

 
Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.

PONDA AIGHARIMU SERIKALI MILIONI 10...!!!


*Usafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
 
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.

 
MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .

Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.

Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.

TSVANGIRAI ATUHUMIWA KUDHARA MAHAKAMA...!!!

Morgan-Tsvangirai_da35d.jpg

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu amesema waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya yanajiri wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
P.T

Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njiya huru na haki. Mugabe alipata asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba kikisema hakikua imani ya kupata haki.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 21, 2013

DSC 0001 5fba2
DSC 0002 b5ca6

RAIS DKT SHEIN AFANYA MABADILIKO YA MAWIZARA ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.

Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya MzeeMarekebisho ya muundo na shughuli katika baadhi ya Wizara ni kama ifuatavyo.

ANGALIA VIDEO YA RAIS KAGAME APOPOLEWA KWA MAWE UINGEREZA


Tuesday, August 20, 2013

AJARI KATIKA MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE DODOMA

DSC00917Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea  katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo


DSC00911 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika ajali iliyotokea  katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa DSC00908Baadhi ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Picha na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma

KIM AITA 24 STARS KUIVAA GAMBIA

Kikosi cha Taifa Stars.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.

Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).

Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).

MWALIMU WA MIAKA 30 AMWEKA KUNYMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 14....!!!


MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Sokoine, Manispaa ya Dodoma (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake David Macha (30).

Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kati ya watoto wanaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania kituo cha Tz 807 FPCT kilichoko Chamwino.

Hata hivyo, katika hali ya  kushangaza Jeshi la Polisi mkoani hapa, limelalamikiwa na wazazi wa mtoto huyo kwa kitendo cha kumlinda mtuhumiwa licha ya kupewa taarifa za uhalifu huo kwa zaidi ya miezi mitano sasa, limeshindwa kumchukulia hatua.

Uchunguzi wa Tanzania Daima ambao umethibitishwa na wazazi wa mwanafunzi huyo, umebaini kuwa mwalimu Macha amekuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miezi mitano sasa.

Wazazi wa mwanafunzi huyo wanathibitisha kuwa kwa zaidi ya miezi mitano, mtoto wao alikuwa na tabia ya kutoroka nyumbani nyakati za usiku na kulala nje, jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka na kuanza kufuatilia nyendo zake.

Walidai kuwa wakati mwingine alikuwa akirudi nyumbani asubuhi kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule na anapoulizwa alikolala, alisema alikuwa katika mkesha.

Akisimulia mkasa huo, mjomba wa mwanafunzi huyo, Silas Mjengi, alisema binti yao anaishi na mama yake pekee katika eneo la Area ‘A’ mjini hapa baada ya mzazi huyo kutengana na mumewe.

"MWAKYEMBE ALINDWE" BARAZA LA VIONGOZI WA DINI


 Mwenyekiti wa baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum

BARAZA la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, limetaka Jeshi la Polisi kumpa ulinzi Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutokana wa ujasiri alioonesha kupambana na dawa za kulevya.


Kutokana na ujasiri huo, Baraza hilo ambalo Mwenyekiti wake ni Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, limempongeza Dk Mwakyembe na kusisitiza umuhimu wa ulinzi huo kwake, kwa kuwa vita aliyoanza, inaweza kuhatarisha usalama wake.
Shekhe Salum alisema hayo jana alipozungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam, akiongeza kuwa kitendo alichofanya waziri huyo kimeonesha uzalendo, ujasiri na upendo alionao kwa Taifa, alilosema linalochungulia kaburi kutokana na dawa hizo.
 

Maombi maalumu
Kutokana na ujasiri huo na hatari inayomkabili Dk Mwakyembe, pamoja na kutaka ulinzi wa Polisi, Shekhe Salum pia aliomba viongozi wa dini wa imani zote, kumwombea kwa uthubutu huo. Alisema watampa ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi anazoonesha ambazo kwa kiasi kikubwa anaamini zitarejesha heshima ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).


“Kwa dhati kabisa Baraza linataka mawaziri na viongozi nchini kuiga mfano wake, ili kuliondoa Taifa letu katika sifa mbaya ya dawa za kulevya,” alisema Shekhe Salum.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, viongozi wana uwezo mkubwa wa kujitolea kupambana na dawa hizo, isipokuwa hakuna aliye tayari kuonesha uthubutu wake, suala alilosema kwa kiasi kikubwa limechangia mapambano dhidi ya dawa hizo kutofanikiwa.

MTANDAO WA KAGAME WAZIDI KUMCHOKOZA KIKWETE.... WADAI MAMA SALMA KIKWETE NI MNYARWANDA...!!!


 Mtandao  wa  News  of  Rwanda  umeendelea  kutuchokonoa  watanzania  ili  kuupima  msimamo  wetu.....

Baada  ya  kukurupuka  na  madai  kwamba  Rais  Kikwete  si  mtanzania  halisi  na  kwamba  ni  mtu  mwenye  asili  ya  Burundi, mtandao  huo  umekuja  na  kioja  kipya....

Taarifa  iliyotolewa  jana  tarehe  19/08/2013  na  mtandao  huo  inadai  kwamba  mke  wa  Rais  Kikwete  aitwaye  Mama  Salma  Kikiwete  ni   mnyarwanda   wa  kabila  la  wahutu ( mhutu )..

Katika  maelezo  yake, mtandao  huo  umeenda  mbali  na  kudai  kuwa  Mama  Salma  Kikwete  ni  binadamu  wa  rais  wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana  na  ndo  maana  rais Kikwete  alitoa  ushauri  wa   mazungumzo  ya  amani  kati  ya  Kagame  na  waasi....

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AUGUST 20, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

VIGOGO WAJUMUISHWA KESI YA LEMA....!!!

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha, John Nanyaro na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Gillis Mroto, leo wanaanza kutoa ushahidi katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema. 
Mashahidi wengine katika kesi hiyo ni, Mkaguzi wa Polisi Bernard Nyambanyana na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane.

Hali kadhalika PC Godfrey na Joachim Mahanyu . Wakili wa Serikali, Elinenya Njiro, alitaja mashahidi wengine watakaotoa ushahidi wao mahakamani kuwa Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu Hamidu, wote kutoka Chuo cha Uhasibu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...