Uamuzi na msimamo wa Japan umetangazwa
jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa
nchi hiyo, Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais
Jakaya Kikwete, Ikulu.
Taarifa ya Ikulu iliyosambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilimnukuu Motegi akisema: "Kwa kuanzia kampuni mbili za Honda na Panasonic zimekubali kujenga viwanda nchini, kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme."
Akaweka msisitizo: "Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais (Kikwete) kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi ya mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la dunia, na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania."