Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.
Tukio
hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la
Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter
lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.