Dar es Salaam. Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa zilizotapakaa kwenye
mitandao kuwa askari wa jeshi hilo waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda
amani,wameanza kujihusisha na makahaba.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa
www.congodrcnews.com wanajeshi wa Tanzania wameanza kujihusisha na
ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.
Taarifa
hizo zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana na
mwanamke mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza shida
zake ambazo ilielezwa alizifanya bila kinga yoyote,askari huyo alikataa
kumlipa ujira wake,hali iliyoleta tafrani na mwanamke huyo kupiga
kelele.
“JWTZ
linapenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo mtupu wenye
nia ya kulipaka matope JWTZ na Tanzania kwa ujumla. “Picha iliyotolewa
kwenye tovuti hiyo ya www.congodrcnews.com ni ya wanajeshi wa Tanzania
walipokuwa katika Operesheni ya huko Comoro mwaka 2008.