
Na Boniface Wambura,
IMEWEKWA MEI 19, 2013 SAA 6:20 MCHANA
MECHI ya watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 imeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.






Mchezaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Simba Abdallah Seseme katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , hivi sasi ni kipindi cha pili na Yanga wanaongoza magoli 2 -0 dhidi ya Simba ambayo imekosa penati katika kipindi cha kwanza wakati mchezaji wake Mussa Mude akipiga vibaya mpira huo baada ya Mrisho Ngassa wa Simba kuangushwa kenye eneo la hatari
Wachezaji wa timu ya Simba na Yanga wakiwania mpira wakati wa mchezo wao unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Baada ya golikipa wa Simba Juma K. Juma kuteswa hali ilikuwa hivi.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata goli la kwanza dhidi ya Simba.













