
Baada ya
Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka
jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana
akamatwe na kushitakiwa.
Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa
habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu
mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa
Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana.
Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani
(NECTA) hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu
akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya
kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa
ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa
Elimu.“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa
kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa,
halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.
Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu
Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa
ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa
sababu ni aibu kwake.







Akizungumza
na mapaparazi wetu kwa njia ya simu jijini Dar juzikati, mrembo huyo
alionesha hali ya kupaniki huku aking’aka na kushangazwa na habari hizo
za ujauzito.







