Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.
Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao
usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu
Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka
kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.
Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa
akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada
maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.
Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda
kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.
“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda
kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda
kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.