Sunday, March 24, 2013

WAZIRI SITTA AWAANIKA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI KUHUSU POSHO

              Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta 
Na: Beatrice Moses
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewajibu wabunge wa Afrika Mashariki akisema wengi hawahudhurii vikao vya kupewa mwongozo kuhusu bunge hilo kwa kuwa “wanataka kulipwa posho”. Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, imekuja siku moja tangu wabunge hao waichongee wizara hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, kwamba imeshindwa kuwapa mwongozo pale wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki. Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo jana, Sitta alisema wabunge hao wamekuwa vinara wa kuomba posho kila
wanapotakiwa kuhudhuria kwenye mikutano ya wizara yake.
Katika maelezo yake Sitta alimeshutumu Katibu wa Wabunge hao, Shyrose Bhanji kuwa ndiye anayeongoza kwa kutoa udhuru mara kadhaa, hivyo kutoudhuria vikao vinavyoitishwa na wizara hiyo.
“ Wizara imejiwekea utaratibu mzuri wa kukutana na wabunge hao, lakini nafikiri katibu wao ndiye anayeongoza kwa kutohudhuria,” alisema Sitta na kuongeza:

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...