Sunday, March 31, 2013

LADY JAYDEE ADAI KUWA CLOUDS FM NI WANAFIKI....WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII


Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

"Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 31.03.2013

.
.
.
.

MLEMAVU AMWANGUKIA WEMA SEPETU

Na. Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA wa kujitegemea  ambaye ni mlemavu wa miguu wa mjini hapa, Elias Ngole Ngoswe amemwangukia msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kwa kumuomba msaada ili aweze kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na mwandishi wetu Jumanne iliyopita, Ngoswe ambaye ulemavu wake ulitokana na kugongwa na gari kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Februari 2, mwaka jana na akavunjika miguu na mfupa wa nyonga, alisema uamuzi wake wa kumuomba msaada Wema unatokana na kuvutiwa kwake na msaada aliompa  msanii mwenzake, Kajala Masanja ambaye alimuokoa kufungwa jela kwa kumtolea faini.
 
“Nimegundua kuwa Wema ana huruma sana nami nikaamua nimuombe msaada kupitia gazeti hili kwani nina matatizo mazito. Nilipovunjika miguu na nyonga nilikimbizwa Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe baadaye nikahamishiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha, nikalazwa miezi mitatu baadaye nilihamishiwa Muhimbili ambako bei niliyoandikiwa nilipe imenishinda,” alisema Ngoswe.

Kwa mujibu wa hati ya malipo ya Muhimbili ya Septemba 10 mwaka jana (nakala tunayo), Ngoswe alitakiwa alipe gharama za matibabu shilingi 9,798,250 ambazo hana.
“Ni fedha nyingi sana ambazo kutokana na ugumu wa maisha, nimeshindwa kulipia. Namuomba Wema na watu wengine wenye huruma wanisaidie ili nitibiwe,” alisema kwa masikitiko Ngoswe. Wema au yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane naye kwa namba 0766 224 284 na Mungu atawabari

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...