Sunday, May 12, 2013

YANGA YATENGA MIL 50 KUMUUA MNYAMA MEI 18

yanga 45743
Yanga
YANGA imeweka fungu la Sh.150 milioni mezani kuwapa motisha wachezaji wake iwapo wataifunga Simba Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mgawo huo kila mchezaji atalamba shilingi milioni tano taslimu.

Hiyo ni kama advansi. Uongozi pia umetenga fungu jingine la Sh.100 milioni kwa ajili ya sherehe za Jangwani baada ya mechi ya Simba, kwenda Bungeni, Dodoma pamoja na Zanzibar.

Awali Yanga walikuwa wamewaahidi wachezaji wake zawadi ya Sh.100 milioni lakini jana Ijumaa Ibrahim Akilimali ambaye ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga alitamka kwamba wameongeza Sh. 50 milioni na kufanya ziwe Sh.150 milioni kwa timu tu.

Hiyo inamaanisha kwamba katika wachezaji 30 kwenye mgawo huo kila mmoja anakunja shilingi milioni tano na chenji chenji.

Akilimali alisisitiza kuwa fungu hilo litahusisha zawadi ya Sh. 70 milioni ya bingwa wa Bara.

Katika hatua nyingine, Yanga imeondoka jana Ijumaa kwa mafungu matatu kuelekea Pemba, Zanzibar kuweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao Kocha Ernest Brandts amesisitiza kuwa anataka mvua ya mabao.

Fungu la kwanza la wachezaji liliondoka asubuhi, la pili likaondoka jioni na la tatu litaondoka leo Jumamosi alfajiri. Kutoka Dar es Salaam mpaka Pemba kwa ndege ni mwendo usiozidi dakika 45. Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 12.05.2013

DSC 0093 d3ab0

DSC 0095 60758

Saturday, May 11, 2013

VIGOGO WA DUBAI WAMGOMBANIA LULU MICHAEL.


ABARI zilizonaswa na mwandishi  wetu  zinaeleza kuwa nyota wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameitwa katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kwa ajili ya kula  bata ikiwa ni pole yake kwa kusota Gereza la Segerea kwa karibu mwaka mmoja.


Chanzo kimoja  kilipenyeza habari kuwa mapedeshee hao wamemualika staa huyo huku ikinyetishwa kwamba, vigogo wa sanaa hiyo Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ndiyo watakaomsindikiza.
 

“Mapedeshee wamemtumia mamilioni ya fedha Lulu, wanataka kufanya naye pati ya pamoja kwa vile ni miongoni mwa mastaa wa Bongo wanaokubalika nchini humo na pia kumpa pole kwa kukaa gerezani muda mrefu.
 

“Mbali na sherehe hiyo, watakapokuwa nchini humo wanatarajia kuendeleza filamu ambayo wameanza kuirekodi hapa Bongo,” kilisema chanzo hicho.
 

Hata hivyo, chanzo kiliweka wazi kwamba kwa sasa, Lulu si rahisi kusafiri nje ya Bongo kwa vile kesi aliyonayo ina mipaka ya sehemu za kwenda. 
Alipotafutwa Dk. Cheni juu ya ishu hiyo, alisema waliomuita Lulu si mapedeshee bali ni Wabongo waishio kule, lakini masharti ya kesi yake hawezi kusafiri nje ya Tanzania.
Dk. Cheni akaulizwa kuhusu yeye na Steve Nyerere kuwepo kwenye safari hiyo ambapo alisema hana ufafanuzi zaidi, akakata simu.

SHEIKHE PONDA ALIPUKA MAISHA YA GEREZANI

Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho. 

Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!

KAULI ZA SHEIKH PONDA.
Alitamka  kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote!

WEMA SEPETU AKISAFIRI KAMA RAIS CHEKI MSAFARA WAKE ULIVYO.........!!!




Wema Sepetu sasa hivi yuko kama rais wa Ngome yake ya Endless Fame filims. Akiwa kwenye safari ya kuelekea Dodoma kwenye party ya uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM Twenzetu na crew yake ya Endless Fame na watu kama PetitMan,TIntyDaddy na Kajala, kwenye gari ambalo yeye yupo ndani yake lilikuwa linapepea kibendelea cha logo ya kampuni yake Endless Fame.

Wema ambaye alitupia Punjab na simple za pink plus black vest, wakiwa njiani kuelekea Dodoma. Walipiga pause na kupiga mapicha kadhaa kadhaa kama kawaida ya Wema siku hizi amekuwa InstaHolic, and kuhusu kutupia kibendera pale mbele nini..nice thing.

WAZIRI ATANGAZA KULIVALIA NJUGA SWALA LA LADY JAY DEE NA RUGE

IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”

Kesi mauji ya Padri Mushi: Nyaraka za siri zavujishwa mahakamani


kurugenzi wa Mashtaka ya Umma Zanzibar,(DPP) Ibrahim Mzee Ibrahim
Nyaraka za barua za mawasiliano kuhusu maendeleo ya jalada la kesi ya mauaji ya Padri Evarist Mushi inayomkabili Omar Mussa Makame, zimevuja baada ya wakili anayemtetea mtuhumiwa huyo kuziwasilisha mahakamani jana mjini Zanzibar.

Barua hizo pamoja na taarifa za kikao kilichofanyika Aprili 4 mwaka huu kujadili jalada la uchunguzi wa kesi hiyo inadaiwa kiliwahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Othman Masoud Othman, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Ibrahim Mzee Ibrahim, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Upelelezi, (DDCI) Yusuph Ilembo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 11.05.2013

2 f5d0e

8 1ad92

6 78892

SHEIK PONDA NA USTAADH MUKADAM WATOA TAMKO KALI LEO


Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho. 
Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!
KAULI ZA SHEIKH PONDA.
Alitamka  kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote! 
Pia kasema ana CD zikionyesha jinsi serikali inavyoua na kupanga kukandamiza uislamu. Kampongeza sana Zitto kabwe kwa mchango wake wa kutetea uislamu bungeni na kamponda yule aliepeleka cd alizoita za uchochezi bungeni! 

Karudia tuhuma za kuwa NECTA kuna udini na Waislamu wanafelishwa! Kasema serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia kuhusu bomu la Arusha kasema, wamekamatwa waarabu ,mbona hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na uislamu! 
Ponda  kasema wakristo hajawahi kuuawa na serikali,ila waislamu 2 ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa.Anadai hata Pemba Waislamu waliuawa na serikali ikitumwa na Kanisa! Amehoji,mbona hatujawahi kusikia mchungaj au padri kauawa?kasema pemba kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini) wakati wanakimbilia Mombasa naTanga.! 

Pia kasema,nchi hii hakuna udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pakusemea

Credit:  JAMIIFORAM

Friday, May 10, 2013

WANAFUNZI WALA KICHAPO KIKALI MARA BAADA YA KUNASWA WAKIJIUZA NJE YA NYUMBA YA KIGOGO WA SERIKALI HUKO SINZA...!!


WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar, waliojitambulisha kwa jina mojamoja, Rachel, Neema na Suzan, wamekumbana na balaa zito baada ya kupokea kibano cha kutosha, Ijumaa lina mkanda kamili.
Tukio hilo lililonaswa laivu na gazeti hili lilitokea maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, usiku wa saa 8:00, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo madenti hao walipokea kibano ‘hevi’ kutoka kwa Polisi Jamii.
Kipondo: Madenti hao baada ya kusurubiwa na Polisi Jamii.
KERO

“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.
Vilio: Warembo hao wakilia baada ya kichapo.
Aliendelea: “Unajua wakikaa hapa ni hatari tupu kwani wanaume wanaokuja kuwafuata wanaweza wakatudhuru kwa sababu hatuwajui.”

SHAFFIH DAUDA MATATANI NA TFF, APEWA SIKU SABA TU ATOE MAJIBU !


Shaffih Dauda
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
 
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.
 
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba

Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA

MAINDA WA BONGO MOVIE AOKOKA KILA MAHALI NA BIBLIA CHEKI PICHA HAPA.


MSANII wa filamu ambaye alikuwa Muislam na baadaye kuamua kuingia kwenye Ukristo na kuokoka, Ruth Suka ‘Mainda’ sasa anaonekana kupambana vilivyo kuhakikisha anaiboresha imani yake kwa kutembea na Biblia kila anakoenda.


Ruth Suka ‘Mainda’ akiwa na Biblia yake mkononi.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Mainda aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa msanii huyo anaonekana kuwa na uchu wa kuijua vilivyo Biblia.

Ruth Suka ‘Mainda’ akisoma Biblia.

“Kwa kweli sasa hivi Mainda hakaukiwi na Biblia mkononi, yeye na Biblia kila wakati. Kuna wakati hata akiwa lokesheni, akipata muda kidogo anaitoa na kuanza kuipitia. Hakika amebadilika,” kilisema chanzo hicho huku maneno hayo yakishibishwa na picha alizotupia Mainda kwenye mtandao wake wa Facebook zikimuonesha akiwa ameshikilia kitabu hicho kitakatifu.

ALIYEJIBADILISHA JINSIA NA KUWA MWANAMKE ATAKA BARAZA LA MTIHANI LISHURUTISHWE KUBADILI VYETI VYAKE NA KUWA NI MWANAMKE



BAADA YA KUJIBADILISHA
MWANAUME aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.


Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti vyake.

DIAMOND PLATZNUM AMKANA MDOGO WAKE WA DAMU!!

Katika pita pita zetu tukutana na kijana aitwaye Saleh Abdul anayedai kuwa ni mdogo wake na Diamond Platnumz. Saleh anadai yeye na Diamond wanachangia baba lakini jitihada zake za kuwa karibu na kaka yake zimekuwa zikigonga mwamba kwakuwa hitmaker huyo anadai kumkana. 

“Mimi ni mtu ambaye nina kipaji cha kuimba lakini najikuta kwamba naambulia patupu yaani kukosa msaada wowote, nikimwendea kaka yangu Diamond anashindwa kunielewa, hataki kunisaidia, halafu wakati mwingine ananikana kabisa kwamba mimi sio mdogo wake,” amesema Saleh kwa uchungu

source bongo5

MAMA KANUMBA: CHONDECHONDE, KABURI LA MWANANGU LISIGEUZWE MTAJI


Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
BAADA ya siku za hivi karibuni kubainika kuwa baadhi ya vijana wanaolinda makaburi ya Kinondoni wamegeuza mtaji kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, mama mzazi Flora Mtegoa amewaomba wahusika kuacha mchezo huo mara moja.
Akizungumza kwa huzuni mama Kanumba alisema alihuzunishwa sana na kitendo hicho cha kaburi la mwanaye kugeuzwa mtaji na kumtaka mtu yeyote atakayetozwa pesa aripoti polisi mara moja.

“Inaniuma sana na naiomba serikali na watu wengine wanisaidie jamani kwa sababu wanaofanya biashara hiyo ya kulipisha watu kwa ajili ya kuliona kaburi wanakosea,” alisema Mama Kanumba.

Hivi karibuni ilibainika kuwa baadhi ya vijana wanaotunza makaburi ya Kinondoni wanatoza shilingi 5,000 kwa watu wanaotoka mikoani kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba na kupiga picha.
Na GP

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...