Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe jana usiku alikuwa katika wakati mgumu wakati Bunge lilipoketi
kama Kamati ya Matumizi, kiasi cha kutishia bajeti ya wizara yake
kukwama. Hata hivyo, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 yalipitishwa.
Wabunge wa vyama vyote walimbana Dk Mwakyembe na
kutoa shilingi karibu katika kila kifungu wakihoji mambo mbalimbali hasa
juu ya mgogoro wa umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda),
uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), usafiri wa majini
hususan usalama wa meli ya Mv Victoria.
Sakata la Uda
Sakata hilo la Uda lilisababisha mvutano baina ya
Naibu Spika, Job Ndugai na Dk Mwakyembe ambaye alilalamikia mjadala wa
Uda kuruhusiwa katika hotuba ya wizara yake. Hata hivyo, Ndugai alipangua hoja hiyo akisema
mbali na kwamba Uda inagusa wizara nyingi, lakini ni suala linalohusu
uchukuzi hivyo ilikuwa sahihi kujadiliwa katika mjadala huo.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla ndiye
aliyeibua suala hilo kwa kuhoji sababu ya Serikali kutoa taarifa
zinazokanganya kuhusu Uda, hali kamati anayoiongoza ilishakaa na pande
zote husika wakiwamo wataalamu na kuwa na hitimisho kwamba Kampuni ya
Simon Group Ltd ni waendeshaji halali wa shirika hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz