Ni kauli ya TCRA ikinukuu sheria ya mawasiliano. Lengo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Profesa John Nkoma,
akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Kampuni za Simu
kuhusu usajili wa laini za simu Dar es Salaam jana.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu
isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda
jela miezi sita.
‘‘Kwa
mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano mteja au muuzaji
wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au
kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa
mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni
lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na
Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi
wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali
kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika
vyombo vya habari.
Katika
maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha
130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba
za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu
yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.
“Katika
vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na Aprili 11 mwaka huu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kampuni zinazotoa huduma za simu za
mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa
namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo
hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa
Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu na vyombo vya
usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na uvunjifu
wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa
ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika jamii.
Pia
alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa
hazitafanya kazi, hivyo watu ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema
namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia 93 na asilimia 7
hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki inatakiwa kuondoka haraka..