Thursday, March 10, 2016

UTUMBUAJI MAJIPU WAOKOA BILLION 700/=

KASI ya kuzuia ukwepaji kodi za Serikali uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na utawala wa Rais Dk. John Magufuli kwa ‘kutumbua majipu’ umeokoa wastani wa Sh bilioni 700.
Katika utawala wa Serikali iliyopita ya awamu ya nne, wastani wa makusanyo ya kodi kwa kiwango cha juu kwa mwezi yalikuwa Sh bilioni 900, lakini baada ya kuingia kwa awamu hii kumekuwapo na ongezeko la zaidi ya Sh bilioni 700 kwa miezi mitatu ya Desemba hadi Februari.
Akitangaza ongezeko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema katika kipindi cha Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh. trilioni 1.4 sawa na ongezeko la wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi.
Alisema kiasi hicho ni kikubwa kikilinganishwa na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba mwaka jana ambapo ilikuwa ni Sh. bilioni 900 kwa mwezi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

'NITAFANYA KAZI NA ALI KIBA BILA VIKWAZO' HARMONIZE

Harmonizeff
LICHA ya tetesi kwamba wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutoonyesha nia ya kushirikiana katika muziki wao, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Bado’, Rajabu Ibrahimu ‘Harmonize’, amesema yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba bila kikwazo chochote.

Msanii huyo alisema Ali Kiba ni msanii wa Tanzania na ni msanii mzuri katika muziki hivyo kufanya naye ‘kolabo’ ni kitu cha kawaida kama wasanii wengine anavyofanya nao.
“Mimi sijui kiukweli kama kuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwa sababu sijawahi kumsikia Diamond akimzungumzia Ali Kiba kwamba wana ugomvi,” alisema Harmonize.

Harmonize ambaye hivi karibuni alijinadi kutoanzisha uhusiano wa kimapenzi, anazidi kujizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake tatu ukiwemo ‘Aiyola’, ‘Kidonda Changu’ na ‘Bado’ huku akizidi kujipanga kwa mambo mengine makubwa yatakayokuja kupitia kampuni ya wasafi anayoifanyia kazi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MKWASA ATAJA SABABU ZA KUMUITA KAZIMOTO

kazimotozKOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amesema uwezo mkubwa aliokuwa nao kiungo wa Simba, ndio umemfanya amuite kwenye kikosi chake kitakachocheza na Chad, Machi 23 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon), utakaochezwa mji wa Djamena, nchini Chad.

Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.

“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

LIVERPOOL KUCHUANA NA MAN U EUROPA

Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja mechi ya Alhamisi ya kombe la Europa kati ya Liverpool na Manchster United kuwa mechi kubwa sana.
Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.

Hatahivyo Klopp anasema :''kila siku kombe la Europa linafurahisha.Ni Mechi kubwa sana.Ijapokuwa sio kubwa zaidi katika kazi yangu kama mkufunzi wa Liverpool lakini ni muhimu sana''.

Manchester United imeshinda makombe 3 ya bara Europa hivi karibuni ikiwa 2008,huku Liverpool ikilibeba kombe hilo mara tano.

Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...