Wednesday, February 10, 2016
WEST HAM YAITUPA NJE LIVERPOOL
Wagonga nyundo wa
London West Ham United imewatupa nje majogoo wa Anfield Liverpool katika
mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.
West Ham walianza
kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio katika dakika ya
45 ya kipindi cha kwanza baada ya kunganisha krosi nzuri Enner
Valencia's
Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa kiungo Philippe Coutinho aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa nyavuni moja kwa moja.
Dakika tisini zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, katika dakika 30, za nyongeza West Ham wakapata bao kupita kwa Angelo Ogbonna,
West Ham watawavaa Blackburn ugenini katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo hapo Februari 21. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)