Mwalimu J. K. Nyerere na aliyekuwa Rais wa Msumbiji marehemu Samora Machel. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Idadi
kubwa ya wabunge nchini Kenya wanajiandaa kuandamana na Rais Uhuru
Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC,Uholanzi ambako anatarajiwa
kuhudhuria kikao maalum kuhusiana na kesi inayomkabili katika mahakama
hiyo.
Kenyatta ametakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo tarehe nane
mwezi huu huku kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda akilalamika kuwa
Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo kuhusiana na ushahidi dhidi
ya Kenyatta. Mapema wiki hii, mahakama hiyo ya ICC ilitupilia
mbali ombi la Rais Kenyatta, la kutaka kikao hicho cha Octoba 8
kuhairishwa au aruhusiwe kutumia video. Majaji wa Mahakama hiyo
walimuagiza Uhuru kufika binafsi mbele yao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Maafisa
wa polisi katikati mwa India wamefutilia mbali harusi kati ya mwanamume
mkristo na mwanamke wa kihindu baada ya shinikizo kutoka kwa makundi ya
kihindu yenye mrengo wa kulia.
Wanandoa hao wawili kutoka Madhya Pradesh walitoroshana na kuoana katika sherehe ya kihindu bila ruhusa ya familia ya msichana. Baada
ya makundi hayo ya Kihindu kupinga hatua hiyo na kutishia kushambulia
majengo ya serikali,maafisa wa polisi katika eneo hilo waliwasaka
wapenzi hao na kuwalazimisha kuachana. Waandishi wanasema kuwa hatua hiyo ya makundi ya kihindu imekuwa ya kawaida katika jimbo hilo katika siku za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Nyota wa Barcelona Lionel Messi anakabiliwa na kesi ya kukwepa kodi,majaji nchini Hispania wamethibitisha tuhuma hizo.
Ikumbukwe Messi alikuwa akikabiliwa na tuhuma za ukwepaji kulipa kodi kwa muda sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz