Thursday, February 21, 2013

Kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara

 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman Kapenjama Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa Kongamano hilo ambalo ni la siku mbili.
Mwenyekiti wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),John Bwire akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia kongamano hilo toka sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.

Simanzi yatawala, Waziri azomewa


Na: Elias Msuya, Zanzibar 
SIMANZI na vilio vilitawala mazishi ya Padri Evarist Mushi yaliyofanyika Kitope Zanzibar jana huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na waombolezaji kutokana na kukerwa na hotuba yake.Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi, Jumapili iliyopita wakati akijiandaa kwenda kuongoza misa katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili mjini hapa. Ibada ya mazishi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ilianza saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili na kuhudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Baada ya misa hiyo iliyomalizika saa 6.30 mchana, msafara wa mazishi ulielekea Kitope yalipo makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Baada ya kufika makaburini, ibada ya mazishi ilianza saa 7.30 mchana na mwili wa Padri uliwekwa kaburini saa moja baadaye. Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa. Waziri Aboud alizomewa kutokana na kauli yake aliyotoa katika salamu za Serikali kuwa kifo cha Padri Mushi ni kazi ya Mungu, ambayo haina makosa. “Serikali imepokea msiba huu kwa
huzuni na masikitiko makubwa. Maumivu ya familia ya marehemu ni maumivu ya Serikali. Padri Mushi ametuachia pengo kubwa lakini kazi ya Mungu haina makosa,” alisema Waziri Aboud kauli ambayo ilipokewa kwa waomboleza kuguna wengine wakizomea hali iliyowafanya baadhi ya viongozi kuwatuliza.
Mmoja wa waombolezaji alisikika akisema: “Kazi ya Mungu ndiyo imewatuma hao wahalifu kuua kwa risasi?”

Mwakilishi wa familia, Francis Mushi alijibu kauli ya waziri huyo alipopewa nafasi ya kutoa salamu kwa kusema: “Tumeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa hasa kwa kuwa Padri hakuugua… Alikuwa kiungo kikubwa katika familia yetu.” Maneno ambayo yaliibua simanzi na vilio kutoka kwa waombolezaji wengi.

Hata Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar, Augustino Shao aliyekuwa amekaa karibu na Rais Dk Shein alipopewa nafasi naye alisema waziwazi: “Naomba kusema kuwa, kauli hii ya mapenzi ya Mungu haipo… Hili ni suala la uovu na tusikubali kushindwa na uovu.” Kauli hiyo ilionekana kuungwa mkono na waumini.

Ibada hiyo ilihitimishwa kwa sala iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga, Antony Banzi.
Wanasiasa waomboleza
Akizungumza baada ya kumalizika kwa msiba huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema wananchi wamechoshwa na kauli za Serikali za kuwatuliza huku watu wakiendelea kuuawa.

“Watanzania tusiendekeze kauli za Serikali za kila siku, eti Bwana ametoa Bwana ametwaa! Kifo cha Padri Mushi hakikutokana na ugonjwa wala Serikali, lakini haiwezekani kila siku Serikali iendelee na ahadi za maneno matupu.
“Haiwezekani Katibu wa Mufti, Fadhili Soraga ajeruhiwe kwa tindikali, Padri ajeruhiwe kwa risasi, kule Geita mchungaji ameuawa na mwaka jana mwandishi wa habari aliuawa na Jeshi la Polisi, tusidanganyane… tuseme ukweli,” alisema Slaa.

Akizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kulitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na vyombo vya nje katika upelelezi, alisema: “Suluhisho siyo kuleta ‘Scotland Yard’ hapa, tatizo letu tunashughulika na matawi wakati mzizi ukiwa bado haujakatwa. Tung’oe mzizi wa tatizo.”

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alivilaumu vyombo vya usalama kwa kushindwa kudhibiti mauaji hayo na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwajibika kwa mauaji yanayoendelea nchini.

“Rais anapoingia madarakani anaapa kuwa mtiifu kwa Katiba na raia wake, lakini haya matukio ya umwagaji damu yamekuwa kawaida sasa. Damu ya mtu ni ya thamani huwezi kuinunua hata uwe tajiri.”

Wananchi watakiwa kwenda kutibiwa Hospitali na siyo kwa waganga wa jadi – Mama Salma Kikwete.



 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili eneo la mkutano wa hadhara, uliofanyika Kata ya Ndoro, Lindi mjini, Feb 20, 2013.
Kina Mama wa Kata ya Ndoro Lindi Mjini, Amina Ali na Saida Ali wakimzawadia kuku, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika, Februari 20, 2013 katika kata hiyo.
 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mama Salma Kikwete, Kata ya Ndoro, Lindi mjini wakishangilia wakati wa mkutano huo.
Wasanii Karim Suleiman ambaye ni mlemavu wa mguu na Mohamed Ali wakionyesha umahiri wao wa kucheza Kiduku katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Mama Salma Kikwete kwenye Kata ya Ndoro, Lindi mjini Februari 20, 2013.
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kuwakabidhi kadi wanachama wapya katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matopeni, Lindi mjini Feb 20, 2013. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
Na Anna Nkinda, Maelezo  Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Lindi mjini  kujenga mazoea ya kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa  mara na kuachana na tabia ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi na kushikana uchawi kutokana na maradhi yanayowasumbua.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alitoa rai hiyo  jana alipokuwa  akiongea kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Matopeni na Wailesi zilizopo wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku saba katika wilaya ya Lindi mjini ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC.
Aliwasihi watu wenye tabia ya kutopenda kupima afya zao wakati wanaumwa na wale wenye tabia za kukimbilia kwa waganga wa jadi huku wakijua fika kuwa ni wagonjwa waache kwani wanaweza kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na kupona.
“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna Ugonjwa wa Ukimwi, muache suala la kushikana uchawi katika hili kwani ugonjwa huu haupatikani kwa kurogwa. Mtu mwenye virusi vya ukimwi  anapimwa  kinga za mwili za kupambana na magonjwa ( CD4) kama zipo chini atapewa dawa za kuongeza na akitumia dawa atakuwa na nguvu na kuweza kufanya kazi zake kama zamani jambo la muhimu asipitishe muda wa kuzitumia” , alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa jamii nzima inahusika katika ulezi wa watoto lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hivi sasa watu wamebadilisha mienendo ya maisha kila mtu anahangaika kulea mwanawe. Na kuwasihi wakazi wa Lindi kufuata maadili ya  zamani ya kuwalea watoto  kwani mtoto wa mwenzako ni wako .
“Ni jukumu la jamii nzima kuwalea watoto wao kwa kufuata  mila za kitanzania , wazazi ambao wakiambiwa kuwa watoto wao wanamienondo mibaya na kuja juu badala ya kuzifanyia kazi taarifa hizo waache tabia hiyo kwani watoto wakilelewa vizuri hata shuleni watakuwa na maadili mazuri na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao”, alisema.
Kuhusu ufanyaji kazi kwa ushirikiano Mama Kikwete aliwataka wananchi hao kuachana na  mambo ya siasa kwani uchaguzi umeshapita hivyo basi wafanye kazi za maendeleo kwa na kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi.
Mama Kikwete alihoji,  “Hawa wazungu manaowaona wanakuja Lindi kufanya kazi wamekuja kujitolea ni jambo la muhimu kujitolea kufanya kazi za maendeleo, ukiambiwa kuna ujenzi wa shule, Zahanati wewe nenda ukajitolee usiseme ile si kazi ya Serikali sasa Serikali ni nani kama si wewe mwananchi?”.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 – 2015 Diwani wa kata ya Matopeni Suleiman Namkoma alisema kuwa idadi ya watoto wanaoanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka 45 hadi 60, kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba kutoka 20 hadi 43, kuongezeka kwa barabara zinazopitika kipindi cha masika na kiangazi na kuimarika kwa miundombinu na barabara za mifereji.
Namkoma alisema, “Tunakabiliwa na changamoto za uchache wa wataalam wa kada mbalimbali ngazi ya kata na jamii kukosa wataaluma wa huduma stahiki, ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa ngazi ya kata, ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, kuchelewa kwa ruzuku ya Serikali kuu na makusanyo madogo ya Halmashauri na upungufu wa walimu wa shule ya msingi”.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mikumbi Zahara Suleiman alisema kuwa katika kata hiyo kuna vikundi vingi vya maendeleo lakini kwa mwaka 2010/2013 hakuna vikundi vilivyokopeshwa na Seambavyo ni  Ayayoli na Mafundi Seremali.
Suleiman alisema, “Tunawashukuru wafadhili waliovikopeshwa baadhi ya vikundi vyetu vya maendeleo kwani  kikundi cha Mwambao Fishing Group kilipewa na Mama Salma Kikwete boti na vifaa vya kuvulia vyenye thamani ya shilini milioni 57  na kikundi cha Uganda kilipewa pesa kutoka MACEP  shilingi milioni 15”.
Katika mkutano wa kata ya Mikumbi   Mjumbe huyo wa NEC aliwapokea vijana 18  waliokuwa wanachama wa CUF na kujiunga  na CCM. Akiwa katika kata za Matopeni, Wailesi  na Mikumbi alikabidhi  kadi  kwa wanachama  wapya wa CCM 43 , Umoja wa vijana 60, Umoja wa Wanawake  22 na Jumuia ya Wazazi  59.

IKULU: Rais Mwai Kibaki awasili nchini kwa Ziara ya Kiserikali (State Visit) ya siku Mbili

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi baaada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili.
Rais Mwai kibaki wa Kenya akikaribishwa  kwa maua na Mwanafunzi Tazmina Rasul(6) muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili huku mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiangalia.Picha na IKULU

SIMBA 1 TZ PRISONS 0



KIKOSI CHA SIMBA

MASHABIKI WA SIMBA

KIKISI CHA TZ PRISONS
MASHABIKI WA PRISONS


WAANDISHI WA HABARI


WAANDISHI WENGINE WAKITUMA STORY ZA MCHEZO HUO KWA KUTUMIA SIMU





WAHUSIKA WA UWANJA HUU WA SOKOINE TUNAOMBA BARABARA HII IWE KATIKA HALI  NZURI HASA ZINAPONYESHA MVUA KWANI HAIFAI KABISA 




PICHA NA MBEYA YETU

Pinda akutana na msimaizi mwendeshaji wa USAID.


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Msimamizi Mwendeshaji wa Shirika la  la Maendeleo la Marekani USAID, Dr. Rajiv Shah kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo wakizungumza na Msimamizi Mwendeshaji wa Shirika  La Maendeleo la Marekani (USAID), DR. Rajiv Shah (kushoto ) na Balozi wa Marekani nchini,  Alfonso Lenhardt Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 20 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...