Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
WAKATI hatua zaidi zikisubiriwa kuchukuliwa kwa watendaji waliohusika
na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza, Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza kuanza kwa awamu ya pili ya
Operesheni hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema wakati wowote Rais Kikwete atatangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya Operesheni Tokomeza na itazingatia haki zote ikiwemo haki za binadamu.
Nyalandu alisema ingawa awamu ya kwanza kulikuwa na kasoro zilizojitokeza, awamu hii ya pili kasoro hizo zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa.
Kusitishwa kwa operesheni hiyo kulikosababisha uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa na waziri mmoja, kujiuzulu kwa mujibu wa Nyalandu, kulisababisha pia tembo 60 kuuliwa.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka jana ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo) huku Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), akijiuzulu.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz