Monday, March 25, 2013

Wema atoa sababu za kutoa milioni 13 za faini ya Kajala

Mrembo Wema Sepetu leo amemake headline baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa leo kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.

Kajala na Wema wakikumbatianaKajala na Wema wakikumbatiana
Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.
“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema.
Wema akwa na KajalaWema akwa na Kajala
“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.”
Kuachiwa kwa Kajala kumepokelewa kwa furaha kubwa na mastaa mbalimbali nchini.

Cpwaa

So I hear Kajala is out! Good news..Hongereni sana wana BOngoMovies! Bongoflava tujipangeni..tutaendelea kupigwa bao kila siku while we are sitting on a Multi-Billion Industry, it’s time to stop fantasizing posing in front of camera poppin bottles of Champagne,Rented Fancy cars,Cheap Wardrobe n ( No..The Ladies are fine,I love them too sitaki ubaguzi)… Tufikirie kibiashara zaidi na sio sifa tu.

Rio Pol

It’s a blessed Monday I say this because finally someone stood up and did something right and righteous. I’ve worked in the entertainment industry for the past seven years and no star or their glam team or entourage would do what Miss Wema Abraham Sepetu did. Thank you god both my girls Elizabeth Michael and Kajala Masanja are free. God bless you wema.
Kajala akikumbatiana na ZamaradiKajala akikumbatiana na Zamaradi
Mboni Masimba
KAJALA outtttttttttt# Mungu mkubwa # WEMA mwokozi wa KAJALA # Mwenyez Mungu akuzdishie na akupe ulipo pungukiwa. Una moyo wa pekee. Lov u always my Dogo
Ben Pol ‏

Nimemvulia kofia Wema, ameni-inspire …moyo kama huo anao mtu mmoja Kati ya Milioni moja, watu hujifanya wakisikitika humu twitter tu…

Elizabeth Michael aka Lulu
Welcome back kay wangu…….Kajala wangu….mamy wangu
Na Bongo5

KAJALA AKILIA KWA FURAHA MARA BAADA YA WEMA SEPETU KULIPA FAINI YA MILIONI 13 MAHAKAMANI LEO

Msanii wa bongo movie Kajala (kushoto) akilia kwa furaha mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu kutoa hukumu ya kesi yake kwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni 13 ambazo zililipwa na Msanii mwenzake Katika tasnia hiyo Wema Abraham Sepetu ili kumnusuru Kajala kwenda jela Miaka Mitano. Pembeni yake aliyemshika ndie Msanii Wema Abraham Sepetu aliyemlipia Faini ya Shilingi Milioni 13 za Kitanzania

Rais Kikwete apokea ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa julius Nyerere toka kwa Rais wa China Xi Jinping

Rais Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya  Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa  Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na  Tanzania.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia
jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za  makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo  jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za  matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na  Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo  wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam  leo. Picha na Freddy Maro - Ikulu.

LOVENESS LOVE ''DIVA'' AJUTA KUGAWA PENZI KWA MO RACKA

Diva alhamisi iliyopita  alifunguka kuhusu kosa kubwa alilolifanya katika maisha yake tangu azaliwe. Na alichosema kajuta ni kua na uhusiano wa kimapenzi na  msanii Mo Racka. Hiki ndicho alichokiandika Twitter jana usiku




WEMA SEPETU AWAFANYIA SHOPPING YA ZAIDI YA TSH. MIL. 6.5 MBWA WAKE WAWILI






Staa wa bongo movie na mmilikiwa kampuni ya Endless love film anayejulikana kama Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amefanya kufuru kwa mbwa wake wawili baada ya ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya TSh. milioni 6.5)

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.
Baada yay eye kuulizwa alikuwa na haya ya kusema
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”
Mbwa hao wa Wema Sepetu aliowapa majina ya Van na Gucc wamekuwa ni gumzo kutokana na jinsi anavyowahudumia huku akiajiri watu maalumu wa kuhakikisha wanavaa, kula na kulala pazuri.

KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5, MUMEWE MIAKA 7

HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Wasanii wa Bongo movie wanazichanga hapahapa kuzilipa ila zimepngua kidogo,Wema na Zamaradi wanakimbia ATM KUZICHUKUA ZINGINE.leo leo Kajala anafika nyumbani kwao

ISHA MASHAUZI NAYE BINGWA WA MADAWA YA KULEVYA AKILI MWENYEWE.......!!!


STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi
Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.

UKWELI KUHUSU ELIMU YA NAIBU WAZIRI WA MH. MLUGO HUU HAPA



Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.

Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.

Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.

“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:

“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”

Waliomfundisha

Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.

Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.

Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.

Chanzo: Mwananchi

CHID BENZ AANZA UGOMVI TENA AMPIGA NGWEA CLUB

                                                            Chid Benz

Rapper Chid Benz, amempiga Cow Bama a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo.ugomvi huo ulitokea baada ya Chid
kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka. Alipoondoka Dully Ngwea akamuuliza inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chid alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chid aliendelea kungea kwa hasira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea
 

MADARAJA MAPYA YA KUFAULU KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE

Serikali kwa kupitia wizara ya elimu imefanya mabadiliko kwenye madaraja ya alama za mitihani ya kidato cha nne. Hapo awali, madaraja yalikuwa ni kama ifuatavyo:

A = 81%-100% 
B = 61%-80% 
C = 41%-60% 
D = 21%-40% 
F = 0%-20% 

Mabadiliko mapya yamefanywa na sasa madaraja MAPYA ni kama ifuatavyo:
A = 80%-100% 
B = 65%-79% 
C = 50%-64% 
D = 35%-49% 
F = 0%-34% 
Taarifa imetolewa mapema ili wanafunzi kwa kidato cha nne waanze kujiandaa vyema na mitihani ijayo

MJUE MWANAMUZIKI ALIYEMTOA KAFARA RAFIKI YAKE ILI APATE UMAARUFU


Baada ya kuvuta bangi, mwanamuziki mmoja nchini marekani (RAPER) anayefahamika kwa jila EL-ARMIN amtoa kafara rafiki yake ili kupata umaarufu, raper huyo aliamini akimuua rafiki yake atapata umaarufu nchini marekani na kupaa kama wasanii maarufu nchini humo. vyombo vya habari nchini marekani vimeripoti kwamba El-armin aliamini kwamba kutoa kafara ni ishara ya mafanikio,

Kabla ya kumuua rafiki yake huyo aliwekea risasi kichwani kwa rafiki yake na kusema  "wewe ni kafara yangu" rafiki yake huyo alizuia pisto  na alijua ni utani. baada ya dakika chache El-armin alimshoot rafiki yake tumboni na rafiki huyo kufa papohapo.

Ndoto zake hatimaye zimepote na amefungwa kifungo cha muda mrefu, masupastaa wakubwa kama 50cent, beyonce, lady gaga,kanye west je huwa wanafanya hivyo?

Mbatia aitaka serikali kuacha kutoa maamuzi ya kibabe na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari.

Na.Mo Blog Team.
Serikali nchini imetakiwa kuacha kufanya mambo bila kutaka ushauri katika masuala ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitalii na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata muafaka wa kweli na ikibidi ivipe ruzuku ili kuhakikisha uendeshaji wa vituo hivyo katika mfumo huo mpya unafanikiwa.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (pichani), ameitaka  Serikali ikubali kwa nia njema kabisa angalau kwa muda wa miezi sita ijayo au hata mwaka mzima ujao kwa mikoa mitatu, kutumia mfumo wa analojia kwa kuwa ndio walikuwa wamejiandaa nao na ndio walikuwa wamesajili nao vyombo hivi ili kujiandaa kuingia kwenye digitali.
Hata hivyo serikali yenyewe imeshatoa tamko kwamba haitorudia nyuma kwenye mfumo wa analojia na badala yake itaendelea kusonga mbele katika mfumo wa digitali kwani tayari mfumo huo ni mfumo wa kiulimwengu.
Suala hilo limeleta changamoto kubwa na wadau mbalimbali wa masuala haya ya habari ambao wametaka kuwepo na mazungumzo ili kuweza kufikia muafaka mzuri katika uendeshaji wa vyombo hivi vya habari kwa kuwa wenyewe wanaona ni mzigo mkubwa kwa sasa kuingia katika mfumo huo wa digitali.

Rais Xi Jinping wa China awasili nchini kwa ziara ya siku mbili apokewa na Rais Jakaya Kikwete

Rais wa China, Mhe. Xi Jinping na mke wake wakiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.
Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika Jukwaa Maalum wakati nyimbo za mataifa yao zilipokuwa zikipigwa sambamba na mizinga 21 kwa heshima ya Mhe. Rais Xi Jinping.
Mhe. Rais Xi Jinping akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa heshima yake.
Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwasalimia baadhi ya kina mama wa Dar es Salaam waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi.
Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na wake zao wakifurahia burudan iliyokuwa ikitolewa na moja ya viku ndi vya burudani vilivyokuwa uwanjani hapo mara baada ya Rais Xi Jinping kuwasili nchini.
Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka uwanjani hapo mara baada ya mapokezi.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...