Tuesday, April 09, 2013
SKENDO YA ASKOFU PENGO KUUZA MADAWA YA KULEVYA YAITIKISA KANISA KATOLIKI............!!!
SKENDO kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, anafanya biashara ya madawa ya kulevya, ilitikisa kisha ikapoa, ila sasa Uwazi lipo kwenye nafasi nzuri ya kupasua jipu.
Januari mwaka jana, Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kutamka hadharani kuwa anaambiwa anauza ‘unga’, kipindi hichohicho, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ambaye alisema wanafanya kazi kisayansi.
“Kama jina la Pengo tunalo kwamba anauza madawa ya kulevya au hatuna, siwezi kutamka kwa sasa, hatutaki kupindisha ushahidi au kuvuruga upelelezi wetu,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, hivi karibuni, Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa vigogo wa jeshi la polisi nchini, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, akasema kuwa suala la Pengo lina utata ila siyo zito.
“Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya,” alisema kigogo huyo.
Aliongeza: “Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya.”...
RAILA ODINGA ASUSIA ZOEZI LA KUPISHWA KWA RAIS WA KENYA NA KUKIMBILIA AFRIKA KUSINI
Inadaiwa Raila Odinga na wagombea wenza wameamua kukwepa kuwepo kwenye kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kuamua kwenda Afrika Kusini .
HILI NDILO POZI LA LULU LA MITEGO KATIKA SIKU YA KUMUENZI KANUMBA
Hii ndo picha ya kimitego imewekwa kwenye instagram na Lulu kwenye siku ya kumuenzi marehemu Kanumba ikiwa ni masaa machache tu baada ya kutoka katika kaburi la marehemu Kanumba.....
MAMA KANUMBA AMSAMEHE LULU YALIYOTOKEA AMWACHIA MUNGU
Mama
wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth
Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa
upande wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia mungu
Akizungumza
katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka
mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi
kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo
humkumbuka mwanaye
Alisema
kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto kwake, mume, rafiki, kaka
alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na alimfanya kuwa karibu kwake
na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo imemfanya kuwa mpweke mpaka leo
SOMA WABUNGE TZ WALIVYOKULA MSOTO JESHINI
Kutoka kushoto: Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid.
WABUNGE
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria
mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
walipata msoto wa nguvu.
HILI NDIO JUMBA LA MILIONI 500 ZA KENYA SERIKALI ALILOMZAWADIWA RAIS MWAI KIBAKI.
.
Wakati Rais mpya wa Kenya
Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa leo kuiongoza nchi hiyo, nimeipata
ripoti ya kituo cha TV cha NTV inayoonyesha jumba lililojengwa na
Serikali ya Kenya kwa ajili ya kumzawadia Rais Kibaki anaestaafu.
Ripoti ya NTV imeamplfy
kwamba kuna uwezekano Rais huyo akaja kuishi kwenye nyumba hii iliyopo
Mweiga Nyeri nchini humo japo pia kuna taarifa nyingine zinaamplfy
kwamba Rais huyo hapendelei maisha ya kijijini, zaidi anapenda mjini.
Mwai Kibaki mwenye umri wa
miaka 81, anamiliki nyumba tatu za kifahari kwenye jiji la Nairobi na
ana nyumba moja nyumbani kwao alikowahi kuwa mbunge.
.Na Millard Ayo
ADHABU YA VIBOKO KURUDISHWA KWA WANAFUNZI KURUDISHWA MASHULENI
Serikali
imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga
nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua
tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa
njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo
Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya
wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo
kienyeji.
“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.
Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”
Uhuru Kenyatta kuapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Kenya.
Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, anaapishwa rasmi leo huku marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakitazamia kuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kwenye sherehe hizo.
Uhuru na mgombea mwenza wake, William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka jana kwa zaidi ya kura milioni 6.13 na hivyo kumshinda mpinzani wake Rail Odinga, aliyepata kura milioni 5.3 .
Uchaguzi huo ulifuatiwa ule wa Desemba mwaka wa 2007 uliomalizika kwa ghasia za kikabila na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine kupoteza makazi.
Kuhusu sherehe, maofisa wa Serikali ya Kenya, walisema zinatazamiwa kuhudhuriwa na viongozi kadhaa barani Afrika na kwamba baadhi yao walianza kuwasili nchini humo tangu jana.
Viongozi
hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameambatana na maofisa
kadhaa wa Serikali yake.Wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais
Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Omar
al-Bashir wa Sudan.
Ziara ya Jay Z na Beyonce nchini Cuba yazua utata kwa baadhi ya wanasiasa nchini Marekani.
Wanasiasa
wawili wa bunge la Kongres la Chama cha Republican nchini Marekani
wamehoji iwapo ziara ya wanamuziki maarufu wa nchi hiyo mume na mke Jay Z
na Beyonce nchini Cuba ilikuwa na kibali cha serikali.
Mastaa
hao wamepigwa picha kadhaa wakiwa mjini Havana wakisalimiana na
mashabiki wao, wakitoka kupata msosi na kutembelea sehemu kadhaa za mji
huo wakati wakisherehekea miaka mitano ya ndoa yao.
Hata
hivyo vikwazo vya kibiashara vya Marekani vinazuia wamerekani
kuitembelea Cuba kwa sababu za kiutalii pekee na anayetaka kusafiri
lazima aombe kibali maalum.
Wanasiasa
hao Ileana Ros-Lehtinen na Mario Diaz-Balart wametuma barua kwa Idara
ya hazina ya Marekani wakiulizia ni aina gani ya kibali walichopewa
wanamuziki hao kuitembelea nchi hiyo.
Wamesema
vikwazo vya kuitembelea nchi hiyo viliwekwa kwa sababu marekani
iliiorodhesha serikali ya Cuba kama taifa linalounga mkono ugaidi na
kudai kuwa nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye rekodi mbaya ya
ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa
kawaida sababu za muhimu zinazoweza kumruhusi raia wa Marekani kwenda
Cuba ni pamoja na matibabu, kusoma, sababu za kidini, huduma za kijamii
na sababi nyingine za kibinadamu.
Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv apatikana.
Masoud
Said (38), mkazi wa Mbeya akifurahia kitita cha Tshs 10,000,000
alizozawadiwa na DStv kwenye campaign ya DStv Rewards. Kila wiki, DStv
wamekuwa wakitoa Tshs 5,000,000 kwenye droo maalum kwa wateja wake
wanaofanya malipo kabla ya akaunti zao kukatika. Kushoto ni Meneja wa
Fedha wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Francis Senguji na Meneja
Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu.
Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv Masoud Said akiwa ameshikilia mabulungutu ya fedha zake.
Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare
POLISI WADAIWA KUMFANYIA UNYAMA KADA WA CHADEMA
HATIMAYE
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba,
amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Nchemba
amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza
video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja
cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho
wakipanga mauaji.
Hata
hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi
lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku
moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu
anayejiita ‘Bukoba Boy’.
MFANYABIASHARA WA KIHINDI AUAWA NA KUPORWA MIL 100, SALENDER BRIDGE
Majambazi
yamempiga risasi mfanyabiashara wa Kihindi na kumuua papo hapo na
kumpora shilingi milioni 100 eneo la Salender Bridge, Upanga Dar es
Salaam jana jioni .
Kwa
mujibu wa walioshuhudia sakata hilo, wanasema mtoto wa kike wa
marehemu pia alipigwa risasi ya paja, lakini akafanikiwa kuendesha gari
lao huku akiwa na mwili wa marehemu babake hadi Hospitali ya Regency.
Hivi sasa msichana huyo shupavu, anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo...
Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kadri tutakavyokuwa tunazipata..
Subscribe to:
Posts (Atom)